Mbunge asiyekuwa na makuu-Kenya

Mbunge asiyekuwa na makuu-Kenya

engmtolera

JF-Expert Member
Joined
Oct 21, 2010
Posts
5,149
Reaction score
1,441
Haya ndiyo maisha ya mbunge Mwahima,hana makuu mzee wa watu,anafuata falsafa ya Mwl Nyerere,maisha yake ni ya kustaajabisha ingawaje ni mbunge ,Wakenya wenyewe wanampenda kutokana na jinsi anavyo ishi

Na Wengi wanamfahamu kama mbunge aliyefanya mtihani wa kidato cha nne akiwa uongozini na uvumi ukaenea kwamba alianguka hata somo la Kiswahili na kupata E,lakini mwenyewe aeleza ilikuwa ni mambo ya vyombo vya Habari

mbunge wa likoni mwalimu masoud mwahima anasisitiza kwamba hataki ukubwa zaidi ya kuwa mbunge ifikapo 2012.

Je wabunge wetu wa Tanzania wataweza kuishi maisha Haya?

<span style="font-family:arial black;"><font size="2"><strong><span class="Apple-style-span" style="font-size: 13px; line-height: 18px; ">
 
Last edited by a moderator:
Kwa hiyo kuishi kifukara ndio mojawapo ya traits za mbunge bora??
 
Kwa hiyo kuishi kifukara ndio mojawapo ya traits za mbunge bora??

kuwa mbunge ya tosha,haina haja ya kufanya biashara,kulidhika na kile ukipatacho ilimradi kinakidhi mahitaji yako

kunahaja gani ya kutuingiza ktk mikataba feki kwa 10%? kwani ukiwa kama huyo mbunge wa kenya utapungukiwa na nini?

tunacho hitaji ni kuishi kwa ule mkate unao kuhusu na sio kutafuta mbinu nyingine za kuongeza kipande cha mkate kwa kutuibia hata kile kidogo tulicho nacho

sijui kama umenipata mkuu
 
huyo hana faida kwani anaeza kuridhika hata nchi yote raia wakiishi kwenye nyumba za nyasi

pooofff

Lakini ukisikiliza kwa makini mtangazaji anasema mbunge huyo amefanya jambo ambalo hata wabunge wasomi waliopita walishindwa kuwafanyia wananchi wa jimbo hilo,

Nadhani maisha yake haya reflect maisha ya wanajimbo,yeye yupo kama yeye na anafanya kile wananchi wanahitaji kufanyiwa
 
huyo hana faida kwani anaeza kuridhika hata nchi yote raia wakiishi kwenye nyumba za nyasi

pooofff

Yeye amekubali kufa maskini kwa kisingizio kwamba mbunge akiwa mfanyabiashara atasahau watu wake. Hata hivo anaonesha ukomo wa upeo wake, huezi kumlaumu sisimizi kwa nini ameshindwa kumeza punje ya mchele..
 
Yeye amekubali kufa maskini kwa kisingizio kwamba mbunge akiwa mfanyabiashara atasahau watu wake. Hata hivo anaonesha ukomo wa upeo wake, huezi kumlaumu sisimizi kwa nini ameshindwa kumeza punje ya mchele..

kwa hiyo unamaanisha hata wale waliotuingiza ktk mikataba feki kwa 10% ni moja ya sisimizi walioweza kumeza punje ya mchele na tusiwalaumu kwa hilo,

hata wale wanaokwepa kulipa kodi kwa kizingizio cha ubunge nao ni sisimizi walioweza kumeza punje ya mchele wasilaumiwe?

wapi tunaelekea?

kwanini sisimizi huyo asimeze vile anavyoweza kumeza tena kulingana na sheria,kanuni na taratibu alizopangiwa yeye sisimizi na sio kuzivunja na kulazimisha kumeza kitu ambacho kinawaacha waliowengi wakifa na njaaa?
 
kenya bado bunge lina falsafa ya kuwakilisha wananchi.
tz ni soko la hisa ndio maana wafanyabiashara wote wachafu tanzania ni wabunge.
 
Back
Top Bottom