Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
"Ifahamike mpaka sasa tunaposimama kama Wabunge wa Mkoa wa Kigoma bado mahitaji yetu hayajatekelezwa ndiyo maana tunasimama kukumbusha na kuieleza Serikali sikivu ili iweze kufahamu namna gani watu wa Kigoma tunahitaji. Mikoa yote ya Tanzania imekwisha kuunganishwa kwa Barabara za Lami, imebaki Kigoma pekee yake" - Mhe. Assa Makanika, Mbunge wa Jimbo la Kigoma Kaskazini
"Tuna Barabara ya Uvinza imeanzia Tabora, kipande cha Tabora kimekamilika kwa Lami lakini kipande kinachounganisha Tabora kutokea Kigoma bado Kilomita 51. Tunaiomba Serikali ya Mama Samia Suluhu Hassan iweze kuona namna bora kutuwezesha watu wa Kigoma tuingie kwenye uchaguzi kipande kiwe kimakamilika"
"Tumeshaieleza Serikali, Barabara kutoka Mwandiga - Kata ya Mwamgongo - Soko la Kimataifa (Kagunga), Barabara imekuwa ni changamoto sana ambapo tangu nimeingia Bungeni nimeipigia kelele nyingi sana. Watu wa Kanda ya Ziwa ni wakati muafaka Serikali iweze kuona namna bora ipeleke miundombinu ya Barabara ili iweze kufika Kata zaidi ya Nne ambazo bado hazijafunguliwa"
"Waziri Bashungwa nimekaa na wewe sana, tumekuja Wizarani kwako tumezungumza na wewe sana kama Wabunge wa Mkoa wa Kigoma. Naomba uweze kuangalia namna bora ambayo tutaweza kuzifungua Kata Nne ili zipate Miundombinu ya Barabara"
"Takwimu za Benki ya Dunia (World Bank) za mwaka 2019 zinaonesha bidhaa ambazo zimepita katika mpaka wa Kigoma zenye thamani ya Dollar Bilioni 600. Mipaka mingine ya Tanga, Mpaka wa Arusha, Oliri, Hololo na Namanga thamani ya fedha zilizopita pale ni Dollar Bilioni 500"
"Mpaka wa Kigoma pekee yake umezipiku mipaka mingine kutokea mwaka 2019. Lakini hadi sasa hali ya Bandari ya Kigoma imekuwa ni kavu sana, ukiangalia utakuta Meli moja tu ndiyo inashusha mizigo. Ukienda upande wa pili utakuta Meli nyingi zinapakia na kushusha mizigo kwaajili ya kuelekea maeneo mengine"
"Hii imesababisha wafanyabiashara wa Kalema, Lubumbashi, na Kabwe (DRC) hivi sasa wanakwenda kupita na kufanya biashara nchi za Burundi na Uganda. Sababu kubwa ni urasimu ambao unaendelea katika Bandari ya Kigoma. Wafanyabiashara wanakwenda Mombasa, Burundi mpaka Rwanda walikuwa wanapitisha mizigo mingi Bandari ya Kigoma"
"Sheria ya kipimo imeweza kuumiza uchumi wa Mkoa wa Kigoma kwa kiwango kikubwa sana. Iko Sheria ya Vipimo vya Habatani inaweza kutanzamwa kwa umakini zaidi kwasababu inachepusha biashara nyingi kwenda nchi Burundi, Rwanda, Uganda na DRC"
"Sheria ya Vipimo vya Habatani inachukua sura ya kwanza ya Sheria ya kipimo ambayo inapima kwa uzito na kwa ukubwa (CBM) ambapo Kodi inayotozwa inaamuliwa na Afisa wa Bandari, jambo ambalo linatoa mianya mikubwa sana. Wafanyabiashara wa nchi hizi wanaikimbia Bandari ya Kigoma kwasababu kumekuwa na urasimu mkubwa"
"Waziri wa Fedha na Wabunge tuangalie namna bora ili tuweze kubadirisha Sheria ya Vipimo vya Habatani ili tuweze kukomboa uchumi wa Kigoma na Bandari ya Kigoma"
"Tumezungumza juu ya Ziwa Tanganyika, hali ya kufunga Ziwa imeumiza uchumi mkubwa wa Wavuvi wengi katika Mkoa wa Kigoma. Imepelekea Uchumi wa watu wetu umezorota kwa kiwango kikubwa. Vimeletwa Vizimba 29 vimejengwa Jimbo la Kigoma Mjini kwenda Ziwani. Jimbo la Kigoma Kaskazini hakuna hata Kizimba kimoja"
"Hali hii imewaingiza wananchi wengi kwenye dimbwi la umasikini kwasababu Ziwa Tanganyika limefungwa. Mkataba wa kufunga Ziwa ulikuwa ni wa zaidi ya nchi 3 mpaka 4. Tunaomba sana Serikali iweze kutazama namna bora kwasababu wananchi waliumizwa, walikuwa na mikopo waliyotoa kwenye Mabenki lakini Ziwa limefungwa na uchumi wao umezorota" - Mhe. Assa Makanika, Mbunge wa Jimbo la Kigoma Kaskazini