Mbunge ataka kusitishwa kuhamasisha matumizi ya pombe na sigara

Mbunge ataka kusitishwa kuhamasisha matumizi ya pombe na sigara

Mkalukungone mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
862
Reaction score
1,755
Leo Mbunge Mwantumu wakati akitoa hoja yake Bungeni ameiomba serikali kusitisha kuhamasisha matumizi ya Pombe na tumbaku ( sigara).

Hoja yake ikajibiwa na Naibu Waziri wa Afya - Dkt.Godwin Mollel kwa kusema kweli mchakato umeanza lakini utaona kwenye sigara na kwenye mambo mengine kweli imehamasisha kwamba ina madhara ya afya sasa suala la kusitisha isitumike kabisa mimi ninachofikiri sio kusitisha kabisa ila ni kila mtu kutambua kwamba ukifanya jambo hili unapata madhara haya.

Vipi hapo wanajukwaa pombe na sigara zisiwepo au mbunge tumpotezee tu?

Nyama ina madhara, chumvi na sukari zina madhara, soda pia ina madhara , waziri mwantum kama vipi ahamie somali kuna marufuku ya pombe kwa sababu za kidini na sio Tanzania nchi ambayo haina dini🤔
 
Leo Mbunge Mwantumu wakati akitoa hoja yake Bungeni ameiomba serikali kusitisha kuhamasisha matumizi ya Pombe na tumbaku ( sigara).

Hoja yake ikajibiwa na Naibu Waziri wa Afya - Dkt.Godwin Mollel kwa kusema kweli mchakato umeanza lakini utaona kwenye sigara na kwenye mambo mengine kweli imehamasisha kwamba ina madhara ya afya sasa suala la kusitisha isitumike kabisa mimi ninachofikiri sio kusitisha kabisa ila ni kila mtu kutambua kwamba ukifanya jambo hili unapata madhara haya.

Vipi hapo wanajukwaa pombe na sigara zisiwepo au mbunge tumpotezee tu?

Nafikiri hoja yake ni ya msingi. Hakuna haja ya kuhamasisha watu kutumia sigara na pombe Bali hii biashara iende kimya kimya kama jinsi biashara ya kitimoto inavyofanyika.

Kitimoto haitangazwi lakini hakuna nyama inayolika zaidi kuliko huyo mdudu. Nafikiri sigara na pombe visihamasishwe Wala kusiwe na matangazo bali mwenye uhitaji atavitafuta mwenyewe na atumie kama anavosema waziri wa afya kwamba kwenye sigara na pombe kuna tahadhari na anayeamua kuvitumia ni ameamua mwenyewe basi iwe vivyohivyo kwenye promotion visiwe promoted Bali mwenye kuvihitaji avitafute mwenyewe.

Promotion ni kama indirect and passive strategy ya ku-trap new users na hata wengine wanajikuta wameingia kwenye huo mtego bila kupenda kwao
 
Back
Top Bottom