JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,780
- 6,607
Mbunge wa Viti Maalumu, Lucy Mayenga ametoa tuhuma kwa baadhi ya wabunge ambao kwa makusudi wanaipotosha Serikali na kuichonganisha na wananchi kuhusu sakata la Loliondo.
Mayenga ametoa shutuma hizo leo Juni 22, 2022 wakati akichangia bajeti kuu ya Serikali, bungeni Jijini Dodoma.
“Machafuko mengi yanayotokea katika nchi hii ni kwa sababu ya kauli za viongozi, kinachoendelea Loliondo na Ngorongoro naomba Serikali iwe makini.
“Wapo wanasiasa wanaingilia hili suala lakini wana maslahi yao, naomba Serikali idili na hao wanasiasa,” anasema Luc.
Amesema lengo la Wabunge hao ni kutaka Rais Samia Suluhu Hassan aonekane hawezi kusimamia vipaumbele na ionekane kuna upigaji ndani ya Serikali, huku akiwataka kuacha tabia hizo.
Ameeleza kuna Wabunge wameandaliwa kupotosha umma suala la Loliondo kwa maslahi yao binafsi.