Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
Mbunge wa Jimbo la Busokelo, Mhe. Atupele Fredy Mwakibete leo Tarehe 10/10/2024 ameunga mkono jitihada za Wazazi na Wananchi katika Ujenzi wa Nyumba ya Mwalimu shule ya Sekondari ya Wavulana Busokelo inayopatikana kata ya Isange kwa Kuchangia pesa Shilingi Milioni 15.
Akiwa katika Mahafali ya pili ya kidato cha Nne kama Mgeni Rasmi, Mhe. Atupele Fredy Mwakibete ameongoza zoezi la changizo kwa wazazi kupitia keki ambapo zaidi ya shilingi Laki Tano zimepatikana.
Aidha, Mhe. Atupele Fredy Mwakibete amesema changamoto zilizotolewa kwenye Taarifa ya Shule ikiwemo ya ukosefu wa Nyumba za walimu jitihada zimeanza kupitia wazazi na yeye kuunga mkono,pia barabara ya kuingia shuleni itarekebishwa na mitambo ya ofisi ya mbunge, suala la maji Mamlaka husika inafanyia kazi pamoja na bwalo la chakula watashauriana na madiwani ili waanze kwa mapato ya ndani lakini kuhusu jengo la Utawala atawasiliana na Waziri wa TAMISEMI ili kupeleka maombi rasmi.
Pia, Mhe. Atupele Fredy Mwakibete ametoa changamoto kwa Mwanafunzi atakayefaulu kwa Daraja la Kwanza (Div 1.7) basi atampatia zawadi ya pesa Shilingi Milioni Moja na Kwa waalimu watakaofaulisha masomo kwa Daraja A watapata zawadi ya Shilingi Laki Moja kwa Kila Somo.