Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
Ikiwa ni muendelezo wa ziara ya Kijiji kwa kijiji ndani ya Jimbo la Busokelo, Mbunge wa Jimbo, Mhe. Atupele Fredy Mwakibete amefika Kijiji cha Ntapisi Kata ya Lupata na kufanya mkutano wa wananchi eneo la Lembuka.
Wananchi wamemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan pamoja na kumpongeza Mbunge wa Busokelo kwa jitihada na kazi kubwa waliyoifanya kwani hawakuwa na huduma za afya na Shule ya Sekondari lakini tayari Zahanati ya Ntapisi imekamilika na inafanya kazi lakini pia Shule mpya ya Sekondari ya Lake Itamba ilikwishaanza pokea wanafunzi na kupunguza adha ya wanafunzi kutembea umbali mrefu kufuata elimu.
Aidha, Mhe. Mwakibete alipokea changamoto mbalimbali ikiwemo waalimu wa Lake Itamba kuomba Mashine za kuchapisha mitihani (Printing Machines), lakini timu mbili za kijijini hapo kuomba mipira pamoja na changamoto za barabara za mitaa.
Akitoa majibu ya changamoto hizo, Mhe. Mbunge amesema kuwa tayari alikwishatoa kompyuta shuleni hapo na kama zitakua zinafanya kazi vizuri basi pia atachangia kwenye suala la printa, lakini pia ameweza kutoa pesa taslimu 160,000/= kwa ajili ya kununua mipira miwili.
Kuhusu changamoto ya Barabara za mitaa, Mbunge Mwakibete amesema kuwa barabara zote zilizo chini ya TARURA zinafanyiwa marekebisho mara baada ya mvua kuisha lakini barabara zilizokosa bajeti zitalimwa kupitia mitambo ambayo Marafiki wameitoa kwa Mbunge.