Mbunge augua ghafla bungeni

Kaitaba

JF-Expert Member
Joined
Jun 30, 2009
Posts
915
Reaction score
54
Ile hali ya kuugua na kuanguka ghafula kwa wabunge iliyokuwa imesimama, sasa imerudi tena baada ya mbunge wa viti maalum Mh, Maria Hewa kuanguka ghafula akiwa bungeni dodoma na kukimbizwa hospitali

Habari zaidi tutazidi kuwaletea
 
Oh ma gad, a hop its not pressure of TAKUKURU queries on doule payments.
 
oooh!
Pole zake...Ninini hii hali huko mjengoni? Au watu wanafukuzia nafasi yake huko jimboni!
 
Haya tupate habari zaidi kutoka gazeti la Alasiri:

CHANZO: ALASIRI
 
Hivi wabunge kwa nafasi zao, huwa wana utaratibu wa kuangalia afya zao mara kwa mara kweli au ndo kama tulivojizoeza? hali kama hii ingeepukwa sana kama tugekuwa na utaratibu huo. naamini kucheki afya kwao sio tatizo kama kwa mwananchi wa kawaida so ni vema wawe wanafanya hivyo!
 
Haya tupate habari zaidi kutoka gazeti la Alasiri:


CHANZO: ALASIRI

Ninavyomfahamu isije kuwa aliyatinga sana MAKALI (Pombe) usiku kucha bila ya msosi, maana ni mpenzi wa konyagiiiiiiiii huyooooooooooooooo wacha. Nampa pole lakini.
 
Ni nadra sana mtu kuanguka au kuumwa "ghafla". Ikitokea hivyo jua mtu alisha kua na matatizo ya kiafya ya muda aidha kwa kujua au kuto kujijua. Ndiyo maana ni muhimu sana kucheki afya kila baada ya muda fulani. Tatizo ni kwamba Watanzania hatuna utamaduni wa regular check ups hata kwa wenye uwezo. Mtu kwenda hospitali mpaka aumwe au aambiwe na daktari awe ana kuja kila baada ya muda fulani.
 
"Alifanya kazi sana na mizunguko mingi ya kikazi bila kupumzika kabla ya kuja mjengoni"
 
duh!! nampa pole sana siwezi kusema zaidi maana sijui zaidi juu yake
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…