Cute Wife
JF-Expert Member
- Nov 17, 2023
- 1,906
- 5,000
Mbunge kutoka Mberee Kaskazini, bwana Geoffrey Ruku amewasilisha Bungeni, muswada utakaowezesha Wakenya kufungwa kwa mwaka mmoja, faini ya Tsh. 2,000,000 (Ksh. 100,00) au vyote kwa pamoja kw awakenya watakaoandamana bila ya kuwa na vibali stahiki.
Kulingana na mswada huo, taarifa ya maandamano inapaswa kutolewa kwa afisa anayesimamia au polisi, pamoja na maelezo ya waandaaji, yakiwemo majina yao kamili, anwani zao za makazi, tarehe zilizopendekezwa, mahali, na muda wa maandamano, ambayo lazima yawe kati ya saa 12 asubuhi na saa 12 jioni.
Aidha, ni polisi pekee ndio watakaokuwa na mamlaka ya kuruhusu au kupiga marufuku maandamano huku wakitoa sababu za uamuzi huo. Kulingana na Mswada huo, waandamanaji pia watazuiliwa kuvaa barakoa au mavazi yoyote yanayoficha nyuso zao au kuzuia utambulisho wao.
Mswada huu umekuja baada ya Wakenya kuupinga vikali Mswada wa Fedha wa mwaka 2024, ambao umesababisha maandamano ya siku nzima siku ya jana Jumanne, Juni 18.
Hali ilivyokuwa kwenye maandamani jana 18 June, 2024
Pia soma:
- Nguvu ya Umma: Bunge lalazimika kubadilisha Muswada wa Sheria ya Fedha baada ya maandamano ya Wananchi
- Yanayojiri Maandamano Kenya kupinga Mswada wa Sheria ya Fedha