Pre GE2025 Mbunge Aysharose Mattembe Agawa Simu Janja 7 (4,500,00) kwa Wilaya za Mkoa wa Singida

Pre GE2025 Mbunge Aysharose Mattembe Agawa Simu Janja 7 (4,500,00) kwa Wilaya za Mkoa wa Singida

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301

WhatsApp Image 2024-05-22 at 17.18.11.jpeg

Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Singida, Mhe. Aysharose Mattembe ametoa Simu Janja 7 (Smartphone 7) na vifaa vya Ofisi za UWT kwa Wilaya Saba za Mkoa wa Singida vyenye thamani ya Shilingi Milioni 4,500,000 na kupokelewa na Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Singida, Ndugu Judith Mwambosa.

Mhe. Aysharose Mattembe amegawa simu Janja hizo ikiwa ni kutekeleza agizo la viongozi wa UWT Taifa kuwataka Wabunge wa Viti Maalum kusaidia watendaji kupata vifaa vya kuendelea na usajili wa wanachama kwenye mfumo wa kielektroniki ili kuongeza idadi ya wanachama wa CCM na UWT.

Mbunge Aysharose Mattembe amegawa sim Janja 7; Kadi za UWT 3000; Vitabu vya Kanuni za UWT 137 ambapo Wilaya ya Manyoni (32), Ikungi (28), Singida Manispaa (18), Singida DC (21), Mkalama (17) na Iramba (20); Lim Paper; Jezi na Pedi kwa Wanafunzi wa kike.

WhatsApp Image 2024-05-22 at 17.18.12.jpeg

Aysharose Mattembe ametembelea Shule Maalum ya Sekondari Solya na kuzungumza na Wanafunzi wa kike ambapo amewapatia zawadi ya Pedi zitakazowasaidia kujisitiri na amewatia moyo na kuwapa hamasa wanafunzi hao huku akiwasisitiza kusoma kwa bidii na kuzingatia lengo lililowaleta ili kutimiza ndoto zao

"Nnyie ndio waasisi wa Shule hii, hivyo mnatakiwa kuwa mfano bora kwa kufaulu vizuri ili kuwapa hamasa wadogo zenu ambao watajaliwa kujiunga na Shule hii hapo baadaye. Nataka kuona ufaulu wa daraja la kwanza kwa nyie wote, nikiwatizama hapa naona wote mnaweza tena mnaweza sana nataka msome kwa bidii ili baadaye mje kuwa viongozi wakubwa kama Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan, inawezekana endapo mtaweka juhudi kubwa katika masomo yenu na kuzingatia maadili" - Mhe. Aysharose Mattembe

Pia, Mhe. Aysharose Mattembe alimshukuru sana Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kwajengea Shule nzuri Watoto wa Singida kwani Shule hiyo maalum ni miongoni mwa Shule kumi za vipaji zilizojengwa nchi nzima na Singida ikiwemo huku akiwapa zawadi wanafunzi hao zikiwemo taulo za taulo za kike na vifaa vya michezo

WhatsApp Image 2024-05-22 at 17.18.18.jpeg

Mwalimu Mkuu, Zainab Mtinda awali akisoma risala yake na kumshukuru Mhe. Aysharose Mattembe kwa kuwajali, Zainab alisema kwa kuwa Shule ni mpya na ipo mbali na maduka ya Stationary, wana changamoto ya ukosefu wa Photocopy, Computer 3 na Maabara za Biolojia, Fizikia na Kemia hazinahazina vifaa vya kutosha vya kujifunzia.

Aidha, Mhe. Aysharose Mattembe ametembelea Hospitali ya Wilaya ya Manyoni na Zahanati ya Salanda kwa lengo la kuangalia ubora wa huduma zinazotolewa huku akiwa amewaplekea wagonjwa na wajawazito Mashuka na Vyandarua.

Vilevile, Aysharose Mattembe ametembelea kikundi cha akina Mama cha Salanda kinachonuaika na mikopo ya Halmashauri ya Asilimia 10 ambapo amezidi kuwapa mikakati na kuwataka kutumia mikopo kama fursa ya kujikomboa kiuchumi na kuwaahidi kuwaleta Maafisa Maendeleo ya Jamii ili kuwapatia mafunzo.
 
Back
Top Bottom