Mbunge Aysharose Mattembe Ashiriki Baraza la UWT Wilaya ya Singida

Mbunge Aysharose Mattembe Ashiriki Baraza la UWT Wilaya ya Singida

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301
Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Mkoa wa Singida, Mhe. Aysharose Mattembe alishiriki na kuwa mgeni rasmi katika Baraza la Kikanuni la Jumuiya ya Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) katika Wilaya ya Singida DC.

Akizungumza katika Baraza hilo, Mhe. Aysharose Mattembe alisisitiza mambo yafuatayo ikiwemo; Kuwataka viongozi wa UWT Wilaya ya Singida kuwahamasisha wanawake wanawaona wanafaa kuchukua fomu na kuwania nafasi mbalimbali za uongozi katika chaguzi za Serikali za Mitaa zitakazofanyika mwenzi Novemba mwaka huu

Mbunge Mattembe pamoja na mambo mengine aliwasisitiza Viongozi wa baraza la UWT (W) ya Singida kuwahimiza wanawake na wananchi katika maeneo yao kwenda Kujiandikisha na kuhakiki taarifa zao kwenye Daftari la Kudumu la Mpiga Kura kwani bila ya kujiandikisha hawatakuwa na fursa ya kupiga kura kuchagua vingozi wanawaotaka

Aidha, Mhe. mbunge Aysharose aliwataka viongozi wa UWT Wilaya ya Singida kuwa mstari wa mbele katika malezi ya watoto wao kuhimiza Wazazi na jamii kuwapa watoto wao malezi na maadili bora ili kupata kizazi kilicho Imara kwa manufaa ya Familia na Tanzania kwa ujumla

Vilevile, Mhe.Mattembe aliendelea kukemea vitendo vya ukatili wa kinjisia vilivyoshamiri katika jamii kwa watoto na Wanawake na kutaka kila mtu kuwa mlinzi wa mwenzake na kuyaripoti haraka matukio kama hayo pindi yanapojitokeza kwenye jamii.

WhatsApp Image 2024-07-24 at 21.20.12.jpeg
WhatsApp Image 2024-07-24 at 21.20.12(1).jpeg
WhatsApp Image 2024-07-24 at 21.20.12(2).jpeg
WhatsApp Image 2024-07-24 at 21.20.14(2).jpeg
WhatsApp Image 2024-07-24 at 21.20.15.jpeg
WhatsApp Image 2024-07-24 at 21.20.15(2).jpeg
WhatsApp Image 2024-07-24 at 21.20.16(1).jpeg
WhatsApp Image 2024-07-24 at 21.20.17(1).jpeg
 
Back
Top Bottom