Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Singida, Mhe. Aysharose Mattembe Katika kusheherekea Siku ya Wanawake Duniani 2024 alipata fursa ya kuwa mgeni rasmi katka sherehe zilizofanyika Tarafa ya Mntinko Wilaya ya Singida.
Mhe. Aysharose Mattembe aligawa Vyeti vya pongezi kwa vikundi vya Wajasiriamali Waliofanya vizuri kwenye mrejesho wa Mikopo ya asilimia 10 katika Mapinduzi Mpambaa Kata ya Mntiko, Mshikamano Mpambaa Kata ya Mntiko, Wavuma Kata ya Ilongero na Upendonako Kata ya Mudida
Akizungumza katika hadhara, Mhe. Aysharose Mattembe amekuwa Mjasilimali aliyepata cheti cha pongezi, Hawa Ayubu Nkumbi wa Kata ya Mntiko amepata cheti kwa kuwa ametumia vizuri mkopo wa Halmashauri na hatimaye ameweza kujikwamua kiuchumi.
Mhe. Aysharose Mattembe alitumia fursa hiyo kuunga mkono agenda ya Rais, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kutumia nishati safi ya kupikia ili kutunza mazingira kwa kugawa majiko ya gesi kwa wanawake wajasiliamali wa tarafa ya Mntinko kwa lengo la kuwapa hamasa ya kuwa mabalozi wazuri wa kutunza mazingira.
Mhe. Aysharose Mattembe amegawa zawadi ya mashuka katika Zahanati ya Mpambaa na Mughanga za Tarafa ya Mntinko ambayo yalikabidhiwa kwa DMO, Grace Ntogwisangu wa Singida DC
Aidha, Mhe. Aysharose Mattembe amemshukuru sana Mkurugenzi wq Singida DC Bi. Esther Chaula na timu yake, Mhe. Diwan Bilal Yusuph wa Kata ya Mntinko, Makamu Mwenyekiti Singida DC Omary Saidi Mande na Waheshimiwa Madiwani wa Viti Maalum wa Wilaya ya Singida kwa kujumuika pamoja katika kusherehekea Siku ya Wanawake Duniani.