Mbunge Boniventura Destery Kiswaga (CCM) Aishauri Serikali Kuongeza Kodi Mafuta Yanayozalishwa Nje

Mbunge Boniventura Destery Kiswaga (CCM) Aishauri Serikali Kuongeza Kodi Mafuta Yanayozalishwa Nje

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301

MBUNGE BONIVENTURA KISWAGA AISHAURI SERIKALI KUONGEZA KODI KWENYE MAFUTA YANAYOZALISHWA NJE

Mbunge wa Jimbo la Magu (CCM), Mhe. Boniventura Destery Kiswaga ameishauri Serikali kuongeza kodi katika mafuta ya kula yanayoagizwa kutoka nje ya nchi na kuondoa Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) kwenye mafuta yanayozalishwa nchini.

Mhe. Bonivetura Kiswaga ameyasema hayo leo Juni 19, 2023 wakati akichangia Bajeti Kuu ya Serikali na Mapendekezo ya Mpango wa Taifa Maendeleo wa mwaka 2023/24.

Mhe. Bonivetura Kiswaga Amesema Serikali imetoa ruzuku katika mafuta na mbegu za mbolea na hivyo kufanya watu wengi kujitokeza kulima alizeti kwenye mikoa mbalimbali ncnini.

"Pamba imelimwa vyakutosha kupitia mikoa 17 inayolima pamba kwa hiyo tuna uhakika wakuwa na mafuta mengi ya kutosha kwenye nchi hii kwa hiyo unapokwenda kutoa kodi kwa mafuta yanayotoka nje unaweka asilimia 25 badala 35 unakwenda kuwafanya wakulima wa nchi hii kuwa masikini" - Mhe. Bonivetura Kiswaga

Amesema halafu Serikali inakwenda kuongeza VAT ya asilimia 18 kwa mafuta yanayozalishwa nchini na kwamba hilo Dk Mwigulu hakushauriwa vizuri na wataalamu wake.

"Naomba nishauri hatuwezi kuongeza ajira kwa wakulima wala katika viwanda vyetu kama kodi ya mafuta yanayotoka nje ya nchi tunazipunguza" - Mhe. Bonivetura Kiswaga

Amependekeza kuwekwa kwa ushuru wa 35 wa mafuta ya kutoka nje ya nchi ili kuhakikisha wakulima Tanzania wanapata mapato ya uhakika.

"Naunga mkono bajeti lakini kwenye hili mheshimiwa waziri nitashika shilingi, kama asilimia 35 haitawekwa kwa mafuta kutoka nje na kuondoa VAT kwa mafuta yanayozalishwa nchini kwa sababu tunakwenda kuwatia umasikini wakulima wa nchi hii" - Bonivetura Kiswaga

mwiguluupiic.jpg
 
Çhama cha Mataahira. Hivi wanajua ndani tuna uwezo wa kuzalisha kiasi mafuta ya alizeti, pamba, samli na mafuta ya karanga?
 
Back
Top Bottom