Pre GE2025 Mbunge Bukoba Mjini: Bilioni 47 kutumika ujenzi wa soko kuu la kisasa la Manispaa ya Bukoba

Pre GE2025 Mbunge Bukoba Mjini: Bilioni 47 kutumika ujenzi wa soko kuu la kisasa la Manispaa ya Bukoba

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

The Watchman

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2023
Posts
896
Reaction score
1,427

Mbunge wa Jimbo la Bukoba Mjini mkoani Kagera, Stephen Byabato, amesema ujenzi wa soko kuu la kisasa la Manispaa ya Bukoba ni miongoni mwa miradi minne iliyopo katika miradi mikubwa ya TACTIC, ambayo itagharimu zaidi ya shilingi bilioni 47, ambapo wafanyabiashara 1,200 watahama kupisha ujenzi wa soko hilo.

Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kutembelea na kukagua miradi hiyo ambayo inatekelezwa katika Manispaa ya Bukoba mkoani Kagera kupitia mradi wa TACTIC, Mbunge Byabato amesema kuwa anaipongeza serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa bilioni 47 ili kutekeleza miradi hiyo ambayo inaenda kuibadilisha Manispaa ya Bukoba na mkoa kwa jumla.

Soma pia: Pre GE2025 Miradi kuelekea Uchaguzi Mkuu: Mhandisi Kundo akagua mradi wa maji unaonufaisha zaidi ya wakazi 200,000 Chalinze

Aidha, ameongeza kuwa ili ujenzi wa soko kuu la Bukoba ukamilike kwa wakati, wafanyabiashara wapato 1,200 waliopo katika soko hilo wanatakiwa kuhamia sehemu nyingine ambazo zimeandaliwa na Manispaa ya Bukoba ili ujenzi wa soko hilo uanze mara moja.

Miradi mingine ambayo itatekelezwa katika Manispaa ya Bukoba kupitia TACTIC ni pamoja na ujenzi wa stendi, kingo za Mto Kanoni pamoja na ujenzi wa barabara zaidi ya kilometa 10 katikati ya mji.


Pia soma ~ Wafanyabiashara Soko la Bukoba wametakiwa kupisha ujenzi lakini hakuna mazingira rafiki waliyowekewa
 
Back
Top Bottom