Mbunge CCM adaiwa kunyang'anywa kadi; Ni njama za kumn'goa Ubunge

Mbunge CCM adaiwa kunyang'anywa kadi; Ni njama za kumn'goa Ubunge

nngu007

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2010
Posts
15,860
Reaction score
5,801
Na Esther Macha, Mbarali

NJAMA za kumng'oa Mbunge wa Jimbo la Mbarali (CCM), Bw. Dickson Kirufi zimeanza baada ya kikao cha Halmashauri Kuu ya Wilaya hiyo kuagizia kumnyang'anya kadi ya uanachama kwa madai ya kuwa chanzo cha mgogoro kati ya wananchi na mwekezaji wa shamba la Mbarali Estate.

Uamuzi huo umefikiwa na kikao kilichofanyika Aprili Mosi mwaka huu katika ukumbi wa Lutherani Kata ya Rujewa kuanzia saa 4:00 hadi saa 10:00 jioni kujadili namna ya kumnyang’anya kadi ya chama mbunge huyo.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti baadhi ya washiriki wa kikao hicho ambao hawakutaka kutajwa majina yao gazetini walisema hatua hiyo imefikiwa baada ya shinikizo la mwenyekiti wa CCM wilaya kuwa na mgogoro binafsi na mbunge huyo na kuchukua mamlaka yake kuwashinikiza
wajumbe kuingia katika maamuzi hayo.

“Sisi hatuna tatizo na mbunge wetu lakini mwenyekiti wa wilaya kaamua kuukuza ugomvi wao binafsi na kuuleta kwetu sisi wajumbe, jambo ambalo hatujawahi kuona,” alisema mmoja wa wajumbe hao.

Taarifa zilizopatikana kutoka kwa wajumbe hao zilisema kuwa ugomvi huo unatokana na Mbuge Kilufi kuwa karibu na wananchi ambao wana mgogoro na mwekezaji wa shamba la Mbarali Estate ambako mwenyekiti huyo wa CCM anafanyia kazi.

Walisema majadiliano hayo yalichukua muda mrefu kumalizika kutokana na pande mbili kutofautiana juu ya maamuzi hayo ambayo yanalenga kumuondolea wadhfa alio nao mbunge kwa kumtoa madarakani.

Walisema kikao hicho kiliwashirikisha baadhi ya wanachama ambao waliandaliwa na mwenyekiti huyo ili kupata nguvu ya kuungwa mkono kwa hoja hiyo.

Hata hivyo, Mpango huo unaodaiwa kuandaliwa muda mrefu kutokana na mwenyekiti huyo kupinga kupita katika kura za maoni kwa mbunge huyo na kumjengea mizengwe katika uchaguzi mkuu wa mwaka jana, licha ya kuwa kundi kubwa la wananchi na viongozi wa CCM wilayani humo wanamkubali mbunge.

“Sisi Mheshimiwa Kirufi ni chaguo letu, lakini taratibu zinazotaka kufanyika tunaona zinaweza kutugawa ndani ya CCM. Wanasema mbunge anachochea mgogoro wa shamba wakati si sahihi kabisa, kwani mbunge ni msuluhishi mkubwa katika mgogoro huo, hata uongozi wa wilaya unaposhindwa," alisema mmoja wa wajumbe hao.

Mbunge huyo alikiri kupata taarifa hizo za kutaka kunyang'anywa kadi ya chama kutoka katika kikao hicho.

“Taarifa hizo nimezipata, lakini tatizo kubwa ni mwenyekiti kuwa na chuki binafsi juu yangu, ni mgogoro wa muda mrefu kwani hata kwenye kampeni zangu hakuwahi kushiriki kama mwenyekiti. Mimi nilidhani baada
ya kumalizika uchaguzi tofauti hizo zitaisha ili tushirikiane kuleta maendeleo kwa wananchi, lakini hali hiyo imekuwa tofauti na mpaka sasa ananiundia mizengwe na kuhakikisha anafanya kila linalowezekana ili kuniondoa madarakani,” alisema.

Alisema hata aliposhinda kura za maoni mwenyekiti huyo aliitisha kikao cha kupinga matokeo hayo na kupeleka mkoani na taifa lakini adhma yake haikufanikiwa, na kuuomba uongozi wa chama Taifa kuliangalia kwa makini tatizo hilo, ambalo linakua kila kukicha kutokana na kuanzia katika ngazi ya uongozi wa wilaya.

Bw. Kirufi alisema yeye ni mbunge wa wananchi wote na siyo baadhi ya kundi la watu kwa maslahi binafsi, na katika migogoro hiyo hahusiki kwani yeye kama mbunge ni lazima awasikilize wananchi wanapolalamika na kufanya hivyo kumemfanya aonekane kama anaratibu vurugu hizo.

“Sijawahi kuitwa ili nipewe taarifa za makosa yangu. Chama changu ni makini kina taratibu zake za kimsingi na madhubuti, kama kuniita, kunihoji juu ya ukiukwaji wangu wa maadili, kunionya kwa barua na hata kunipa nafasi ya kujieleza kwa maandishi.

"Kinaweza kusikiliza utetezi wangu na kama nina makosa kinaweza kunipa adhabu ya kujirekebisha, lakini hayo yote sijahusishwa na ninasikia tu, hizo ni chuki binafsi za baadhi ya viongozi wa chama, hasa mwenyekiti wangu.

Katibu wa CCM Wilaya ya Mbarali, Bw. Mkanyege Kashiririka alipotakiwa kuzungumzia tatizo hilo alisema jambo hilo msemaji wake ni mwenyekiti wa CCM wilaya, Bw. Ignas Mgao ambaye alidai kuwa hana ugomvi wowote na mbunge.

Kuhusu kutoshiriki katika kampeni za mbunge huyo alisema katiba ya chama haimruhusu kuingia katika kampeni bali ni sekretarieti ya chama ndo inahusika.
 
CCM Viongozi wenye Madaraka ni Wengi
 
mmh! siamin km mafisadi wanafanyiana mbaya!
 
Watamkosa huyo mbunge chaguo la wananchi wengi shauri yao watajuta hao viongozi watapoteza mvuto kwa uongozi wa juu jimbo likichukuliwa shauri yao....acha wafanye upuuzi wao waone!!
 
SKILLSFOREVER......you have said it.......CCM ilipoteza majimbo mengi si kwa sababu upinzani ulikuwa na nguvu...no. hapana ni sababu ya chuki zao binafsi ndani kwa ndani
 
hawasisiem hawana kuchukuliana hatua kwao sababu hata m/kiti wao ni mtu wa washkaji...wanachuliana poa,hii ita wa cost
 
Back
Top Bottom