Hivi tunakwenda wapi sasa? What a dumbest way of protest!
12/20/2008 4:11:56 AM
12/20/2008 4:11:56 AM
Source: NifahamisheKATIKA hali inayoashiria kukua kwa uhasama miongoni mwa viongozi wa chama cha Mapinduzi Mkoani Mbeya, Mbunge mmoja wa viti maalumu anadaiwa kumdhalilisha kiongozi mwenzake kwa kutaka kumvisha nguo yake ya ndani wakati wa kikao cha kamati ya siasa
Taarifa za ndani za kikao zinadai kuwa mbunge huyo alifanya kituko hicho katika kikao cha Desemba 17,mwaka huu, kwa kutoa nguo za ndani kutoka kwenye mkoba wake wa mkononi na kuwanyooshea wajumbe wa kikao hicho.
Vyanzo vya habari kutoka ndani ya kikao hicho vinadai kuwa mbunge huyo alikuwa akimtuhumu mwenyekiti wa moja ya jumuiya za CCM kwamba anapiga vita harakati zake za kuwania uongozi katika chama hicho.
"Wakati akimtuhumu mwenyekiti wa huyo wa moja ya jumuiya za chama hicho ndipo kwa mshangao alitoa nguo hiyo ya ndani kutoka katika pochi yake na kutaka kumvisha mwenyekiti mwenzake huyo ambaye ni mwanaume"
Habari zaidi zinadai mwenyekiti huyo ya jumuiya ambaye ni mgeni katika kikao hicho alichukizwa na kitendo hicho hivyo kuja juu baada ya kuona anadhalilishwa.
Hata hivyo kabla hajachukua hatua zaidi mwenyekiti wa CCM mkoani humo, Nawab Mulla aliingilia kati na kwa kutumia busara alimuonya mbunge huyo kwa kitendo chake kisicho cha maadaili kwa chama hicho.
Mulla alimtaka mbunge huyo kumuomba radhi mwenyekiti aliyemdhalilisha hali iliyomshawishi aliyedhaliliwa kutuliza jazba.
Baadhi ya wajumbe waliokuwa katika kikao hicho ambaye hawakupenda kutajwa majina yao walisema mbunge huyo alikuwa anaheshimiwa sana mkoani humo, alijivunjia heshima mbele ya wajumbe wa kikao hicho ambao baadhi ni sawa na wajukuu zake" alisema