Mbunge Chege awajengea uwezo Madiwani kuelekea maboresho ya Daftari la Mpiga Kura

Mbunge Chege awajengea uwezo Madiwani kuelekea maboresho ya Daftari la Mpiga Kura

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301
Wakati serikali ikitarajia kutangaza zoezi la maboresho ya daftari la wapigakura katikati ya mwezi wa saba kwaajili ya uchaguzi wa serikali za mitaa utakaofanyika mwishoni mwa mwaka huu Mbunge wa Jimbo la Rorya Mkoani Mara @jafari_chege anatarajia kuanza ziara itajayojikita kata kuwaanda wananchi wa jimbo hilo kujiandaa na zoezi hilo la kitaifa.

Baada ya kuahirishwa kwa vikao vya bunge la bajeti June 28 mwaka huu hatimaye imefungua mlango kwa mbunge wa jimbo la Rorya Jafari Chege kirejea jimboni kwaajili ya ziara yenye lengo la kutoa elimu na kuwaandaa wananchi na zoezi la kuboresha majina kwaajili ya uchaguzi wa serikali za mitaa.

Chege ameanza zoezi hilo kwa kukutana na madiwani na kuwajengea uwezo ili wawe na uelewa wa pamoja juu ya namna wanavyoweza kuwaeleimisha wananchi kujitokeza pindi milango ya maboresho itakapofunguliwa pamoja na kushiriki uchaguzi kikamilifu.

 
Back
Top Bottom