Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
MBUNGE CHEREHANI AKABIDHI MADIRISHA 15 (MILIONI 4) KUKAMILISHA NYUMBA YA KATIBU WA UWT WILAYA YA KAHAMA
Mbunge wa Jimbo la Ushetu Mhe.Dkt Emmanuel Cherehani amekabidhi Madirisha 15 yenye thamani ya TZS. Milioni 4,162,000/- kukamilisha nyumba ya Katibu wa Umoja wa Wanawake Tanzania UWT Wilaya Kahama mkoani Shinyanga.
Cherehani amekabidhi Madirisha hayo kwa Mwenyekiti wa UWT Wilaya ya Kahama Theresphora Salia (kushoto) na Katibu Happyness Mpena(Kulia) leo Agosti 12, 2023 katika Mtaa wa Shunu kata ya Nyahanga.
Huu ndio muonekano mpya Shule ya Msingi Butibu iliyopo Kata ya Kinamapula Halmashauri ya Ushetu mkoani Shinyanga ambayo iliezuliwa kwa upepo na kupelekea kuwepo uhaba wa vyumba vya madarasa kwenye Shule hiyo na Wanafunzi kulazimika kusomea chini ya mti.
Kufuatia Changamoto hiyo kupitia jitihada za Mbuge wa Ushetu Dkt. Emmanuel Cherehani, Serikali ilitenga kiasi cha Shilingi 145 kwaajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa 5 na pesa iliyobaki ikakamilisha ujenzi wa vyumba vingine 4 vya madarasa ambavyo vilijengwa kupitia nguvu za Wananchi mpaka hatua ya boma.
Attachments
-
F3W2l-SXAAA_QK0.jpg71.8 KB · Views: 4 -
F3W2l-WWoAEHvXM.jpg54.6 KB · Views: 4 -
F3W2l-SWwAABVrW.jpg57.8 KB · Views: 4 -
WhatsApp Image 2023-08-13 at 14.01.17.jpeg55.3 KB · Views: 5 -
WhatsApp Image 2023-08-13 at 14.01.19(1).jpeg24.7 KB · Views: 5 -
WhatsApp Image 2023-08-13 at 14.01.17(1).jpeg26.1 KB · Views: 5