Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
MBUNGE CHEREHANI: WALIMU TUSHIKAMANE KUTOKOMEZA ZERO USHETU
Mbunge wa Jimbo la Ushetu, Mhe. Emmanuel Cherehani amewataka walimu wa Shule za Sekondari katika Halmashauri ya Ushetu mkoani Shinyanga kuongeza jitihada ufaulu kwa Wanafunzi wote ili kutokomeza alama sifuri.
Rai hiyo ameitoa jana katika hafla fupi ya kuwapongeza watumishi hao kwa kuongeza ufaulu kwa kipindi kifupi ambapo amesema "Taifa ambalo litakuwa kipaumbele kwenye elimu na kuelimisha watu wake ni taifa ambalo litasonga mbele kiuchumi"
Aidha, Cherehani amewataka kuitunza miundombinu ya Shule itakayochochea upatikanaji wa elimu bora huku baadhi ya walimu wakipongeza hafla hiyo iliyoandaliwa na mbunge huyo na kuahidi kuongeza kuongeza ufaulu