Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
MBUNGE CHRISTINA MNZAVA AZINDUA UANDIKISHAJI DAFTARI LA KUDUMU LA MPIGA KURA WILAYANI KAHAMA
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Dkt. Christina Christopher Mnzava ameshiriki katika Uzinduzi wa Zoezi la Kujiandikisha katika Daftari la Kudumu la Mpiga Kura Wilaya ya Kahama Mkoa wa Shinyanga akishirikiana na viongozi mbalimbali wa UWT Wilaya ya Kahama.
Mhe. Christina Mnzava amesema kuwa lengo la kuzindua zoezi la Daftari la Kudumu la Mpiga Kura ni ili kuwafikia na Kuhamasisha wananchi wote kwenye Mashina kujitokeza kujiandikisha na kuhakiki taarifa zao kwenye daftari la mpiga kura.
Mhe. Christina Mnzava amewaambia Wanawake watumie fursa na haki yao ya kuchagua na kuchaguliwa na wajitokeze kuwania nafasi kwenye Mitaa, Vitongoji na Vijiji ili kuwa uwakilishi wa Wanawake katika nafasi mbalimbali za uongozi.
Katika Mikutano yote ya hadhara aliyofanya, Mbunge Christina Mnzava ameendesha zoezi la
kusajiri wanachama wapya katika mfumo wa kielektroniki; Ameelezea mambo yaliyofanywa na Rais (Utekelezaji wa Ilani ya CCM); Kusikiliza kero na kuzifanyia kazi.