Mbunge Condester ataka gongo ihalalishwe, aenda bungeni na 'sample'

Mbunge Condester ataka gongo ihalalishwe, aenda bungeni na 'sample'

Magazetini

JF-Expert Member
Joined
Aug 16, 2014
Posts
593
Reaction score
1,712
Condester Sichalwe(Momba): Ni nini watu wa TBS wanaweza wakatusaidia kutoa makali ambayo yapo kwenye gongo yafanane konyagi, yafanane na pombe nyingine ambazo mnaziona za kifahari ambazo matajiri wanakunywa lakini wote wakinywa wanalewa.

Nataka kuwaambia, pombe hizi za kienyeji ambazo mmezidharau, wapo wafanyabiashara wakubwa na mashughuli, bibi zao, shangazi zao, mama zao wamewasomesha kupitia hizi pombe za kienyeji, wapo wabunge. Prof. Kitila Mkumbo amesema amesomeshwa na bibi yake kupitia pombe za kienyeji.

Nimekuja na sample za pombe za bei rahisi(Anazionesha)
 
Alitakiwa abebe na Kimpumu. Maana inatumika sana huko Mbeya na Songwe.

Tunasubiri na Wabunge wa Korogwe nao waende na pombe zote za kienyeji za Wilaya hiyo! Kuanzia denge, Boha, Kangara, gongo ya miwa, Mnazi, nk.
 
Japo mimi naona unywaji pombe ni ubatili na dhambi lakini naiona hoja ya mbunge. Hizi za urusi zinaitwa spirit ni sawa tu na hizo.
 
Back
Top Bottom