Mbunge wa Jimbo la Momba Mhe. Condester Sichalwe amewataka wananchi kutokushawishika na watu wanaotoa rushwa ikiwemo kuwanunulia pombe ili wakawapigie kura, bali wanapaswa kupima maendeleo yaliyofanyika katika kipindi chake cha miaka minne kulinganisha na miaka 15 iliyopita.
Mhe. Condester ametoa wito huo akiwa katika kijiji cha Masanyinta wakati wa ziara yake ya kuzindua miradi ya maendeleo iliyotekelezwa Jimboni humo ambayo ni ujenzi wa vyumba vya madarasa shule ya msingi Chiwanda, Josho la mifugo Chitete na miundombinu ya kutolea huduma za Afya Zahanati ya Masanyinta.