Pre GE2025 Mbunge Condester Sichalwe Anunua "Division One" kwa 100,000 na Alama "A" kwa 10,000

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301

WhatsApp Image 2024-07-09 at 06.34.23.jpeg

Mbunge wa Jimbo la Momba, Condester Sichalwe (Mundy) ameendeleza kampeni yake ya kutembelea shule mbalimbali za Sekondari zilizopo ndani ya Halmashauri ya Momba kwaajili ya kunadi sera yake ya kununua Division one na alama ya “A” kwa masomo ya Sayansi na Sanaa kwa kidato cha pili na cha Nne.

Akiwa katika ziara yake ya kusikiliza na kutatua kero za wananchi, leo Julai 8, 2024 amefika shule ya Sekondari kata ya Chilulumo, na kutambulisha mpango huo kwa wanafunzi na walimu, ikiwa ni moja ya njia ya kuhamasisha wanafunzi kujituma katikaa masomo na kupandisha kiwango cha taaluma ndani ya jimbo lake.

“Nimekuja na mpango/ kampeni ya kununua division one kwa shilingi laki moja (tsh.100,000) na alama ya “A”, kwa shilingi elfu kumi (10,000) lakini kwenye kununua division one nitaswapu na division “0” kwamfano kama kutakuwa na Division one 20 nitatoa milioni mbili, lakini kama kuna “0” kumini nitaswapu na kuwapa milioni 10, kwamaana hiyo mtanirudishia milioni kumi zangu zilizotokana na sifuri.” Sichalwe.

Pia soma: Uzi Maalum wa Vibweka na Hekaheka za wanasiasa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

Akizungumza kwaniaba ya wanafunzi , Mkuu wa shule ya Sekondari Chilulumo Mwalimu Charles Siwakwi amesema mpango huo ni mzuri kwani utasaidia kuleta motesha na ushindani mkubwa kwa wanafunzi kusoma kwa bidiii na kuzingatia yale yote yanayofundishwa na walimu wao.

Katika hatua nyingine Sichalwe amehimiza walimu na wanafunzi kuangalia uwezekano wa kupanda miti ya mikorosho katika mashamba ya shule na majumbani mwao ili iwe ni njia moja wapo ya kujiongezea vipato.

Aidha Mbunge Sichalwe amewaahidi wanafunzi hao endapo watapata division one kuanzi ishirini na kuendelea kwa kidato cha pili na cha Nne atawapa mwaliko maalumu wa kwenda Bungeni Jijini Dodoma.
 
Elimu imekwisha, taifa limekwisha ...it's over

1000011205.jpg
 
Ujinga mtupu, Division one ndio elimu?
 
Back
Top Bottom