Mbunge Condester Sichalwe - Wakulima Undeni Vikundi vya Ushirika Ili Mkopesheke Kwenye Mabenki

Mbunge Condester Sichalwe - Wakulima Undeni Vikundi vya Ushirika Ili Mkopesheke Kwenye Mabenki

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301
Mbunge wa Jimbo la Momba Mkoa wa Songwe Condester Mundy Michael Sichalwe tarehe 22 Julai, 2023 ameendelea na ziara katika Kijiji cha Yala na kuzungumza na wakulima wa Kijiji hicho.​

Akizungumza katika Mkutano wa hadhara wa wananchi, Afisa Kilimo cha Yala amesisitiza wananchi kutumia na kulima Kilimo chenye tija ili kuwa na mazao mengi huku akiainisha jiografia, mbolea na mbegu za kutumia kuendana na msimu wa Kilimo.

Condester Sichalwe amewasisitiza Mabalozi wa Vitongoji na Wenyeviti wa Vijiji kuhakikisha wanawatambua watu wote wanaokuja kuishi ndani ya maeneo yao ili iwe rahisi kutambua nani mgeni na nani mwenyeji huku akiwasisitiza kufikisha taarifa kwa wananchi wao.

Mhe. Condester Sichalwe amesema Serikali imejitahidi kutekeleza majukumu yake ikiwemo Kusambaza Umeme Vijijini (REA), Hospitali, Shule na Skimu za Umwagiliaji huku akiwataka wananchi kuzitumia fursa zinazoletwa na Serikali kwa manufaa yao na nchi.

Mhe. Condester Sichalwe amewashauri wananchi kuunda vikundi vya ushirika ili wavitumie kama dhamana ya kuchukua mikopo kutoka Wizara ya Kilimo kwani wananchi wengi wamekuwa hawakopesheki kwa sababu hawana mali za kuweka dhamana kwaajili ya kukopa

Mhe. Condester Sichalwe amesema kuwa Wataalam kutoka Wizara ya Kilimo watafika katika Vijiji vyote vya Jimbo la Momba kwaajili ya kutoa elimu kuhusu mambo yote ya Kilimo ili wakulima wa Kijiji cha Yala wawe na Kilimo chenye tija.

Wananchi wa Kijiji cha Yala wamemshukuru Mbunge na Serikali kwa kujenga Madarasa Mawili na Ofisi, ujenzi wa soko, Skimu ya umwagiliaji, umeme kuwafikia Vijijini huku wengi wakisisitiza umaliziaji wa Zahanati, ujenzi wa nyumba za Walimu na upungufu wa walimu katika shule.

Diwani wa Viti Maalum amemshukuru na kumpongeza Mbunge wa Jimbo la Momba Mhe. Condester Sichalwe kwa kuwachangia Shilingi Milioni 2 (2,000,000) kwaajili ya ujenzi wa Zahanati na soko.

Diwani wa Kata ya Chitete amesema kuwa Serikali imepeleka Shilingi Milioni Hamsini (50,000,000) kwaajili ya ujenzi wa Zahanati ya Kata, na ujenzi wa Shule mpya Namingong'o na Yala.

Mwisho, Mhe. Condester Sichalwe amesema atawaleta watu wa TASAF Kijijini hapo huku akisema atafuatilia kwanini wananchi wamechangishwa fedha za NIDA na kujua ni lini vitambulisho vyao vitaletwa.

Mbunge Condester Sichalwe amesema ataendelea kufuatilia suala la kuwa na walimu wa kutosha na kuwasisitiza Madiwani na viongozi wa Vitongoji kusimamia vizuri fedha za miradi inayoletwa na Serikali kwa ajili ya kuboresha huduma.
 
Back
Top Bottom