Mbunge Condester: Takwimu za Sensa Zitumike Kutoa Mikopo

Mbunge Condester: Takwimu za Sensa Zitumike Kutoa Mikopo

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301
Mbunge wa Jimbo la Momba Condester Sichalwe ametoa wito kwa Taasisi za kifedha Mkoani Songwe kutumia Takwimu za Sensa kutoa mikopo kwa wakulima.

Ametoa wito huo katika Kongamano maalum lililofanyika Wilayani Momba Mkoani Songwe la kuwawezesha kiuchumi wakulima ambapo amesema Taasisi za kifedha wanapaswa kuwakopesha wakulima ili na wao wajikwamie kiuchumi.

Aidha ameomba Chama kikuu cha ushirika Mkoani humo kuwajibika kama Chama ili kuwasaidia kuwakopesha wakulima kutokana na mazao waliyonunua kutoka kwa wakulima.

Kongamano hilo limewakutanisha Wadau mbalimbali wa maendeleo zikiwepo Taasisi za kifedha ili kutanua wigo wa kutambua fursa za kiuchumi kwa Vijana wa Jimbo la Momba na baadhi ya watumishi

WhatsApp Image 2024-07-22 at 06.33.02.jpeg
WhatsApp Image 2024-07-22 at 06.33.03.jpeg
WhatsApp Image 2024-07-22 at 06.33.03(1).jpeg
WhatsApp Image 2024-07-22 at 06.33.04.jpeg
WhatsApp Image 2024-07-22 at 06.33.06.jpeg
 
Back
Top Bottom