Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
MBUNGE DAVID MATHAYO ATOA MILIONI MBILI UKARABATI WA SHULE YA MSINGI KITAMRI
Shule ya Msingi Kitamri iliyopo katika Kata ya Stesheni, wilayani Same mkoani Kilimanjaro inakabiliwa na Uchakavu wa majengo pamoja upungufu wa vyumba vya madarasa hali inayowafanya Wanafunzi kusoma kwa zamu.
Kwa sasa shule hiyo ina madarasa sita ya kujifunzia, ambapo kwa sasa wamelazimika kubadili Stoo kuwa darasa.
Mkuu wa Shule hiyo Hadija Rajabu anasema kwa sasa wana Wanafunzi 264, Wa darasa la awali hadi darasa la saba.
Ameiomba Serikali na Wadau wengine kusaidia kukabiliana na hali hiyo kwani hata ruzuku wanapokea 45000 kwa mwezi ambayo haitoshi kwenye ukarabati.
Heriel Mjema Diwani Kata ya Stesheni anasema shule hiyo inahitaji ukarabati mkubwa.
Hali hiyo imemgusa Mbunge wa Jimbo la Same Magharibi Dkt David Mathayo ambaye ametoa kiasi cha milioni mbili kwaajili ya kukarabatiwa kwa madarasa hayo.