Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
WANANCHI PWANI WAHAMASISHWA KUSHIRIKI KAMPENI YA MSAADA WA KISHERIA YA MAMA SAMIA
Mbunge wa Viti Maalum, Dkt. Alice Karungi Kaijage, amewataka wakazi wa Pwani kushiriki kikamilifu Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia, akisema kuwa kampeni hiyo imeleta manufaa makubwa kwa wananchi katika mikoa zaidi ya 15 nchini.
Akizungumza siku ya Jumatatu Februari 24, 2025 katika uzinduzi wa kampeni hiyo uliofanyika katika Kata ya Maili Moja, kwenye Uwanja wa Stendi ya Zamani, Dkt. Karungi amewahimiza wananchi kuitumia fursa hiyo bure ili kupata suluhisho la changamoto zao za kisheria, ikiwemo migogoro ya ardhi na mirathi.
Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025
"Hakika ninawaambieni watu wa Pwani, kampeni hii imefanyika katika mikoa isiyopungua 15 na matunda yake ni makubwa sana. Ninawaomba Wanapwani tuwaambie wenzetu waje, huduma hii ni bure," amesema.
Ameongeza kuwa msaada wa kisheria unaotolewa kupitia kampeni hiyo umewapa matumaini wananchi wengi, hasa wale wasio na uwezo wa kugharamia huduma za kisheria.
"Katika mikoa tuliyopita, kampeni hii imeleta matumaini makubwa kwa wananchi wanyonge katika kutatua migogoro yao mbalimbali. Wananchi mliopo hapa na mliopo kwenye mabanda mbalimbali, nendeni majumbani mkawahamasisheni wenzenu. Migogoro ya ardhi, mirathi, na mambo mengine yanatatuliwa hapa kwa hisani ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan," amesisitiza Dkt. Karungi.