Mbunge Dkt. Florence Samizi Aiomba Serikali Kuongeza Bajeti ya TARURA Jimbo la Muhambwe

Mbunge Dkt. Florence Samizi Aiomba Serikali Kuongeza Bajeti ya TARURA Jimbo la Muhambwe

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301
ZIARA YA ya MAKAMU WA RAIS MKOANI KIGOMA - Mkutano wa Hadhara Kata ya Makere, Muhambwe

Mbunge wa Jimbo la Muhambwe, Mhe. Dkt. Florence Samizi amesema kuwa Jimbo la Muhambwe linaongoza kwa uzalishaji wa Mihogo lakini kwasasa kuna potoki la bei ya Mhogo

Mhe. Dkt. Florence Samizi amesema kuwa anaiomba Serikali kuratibu biashara ya ujirani mwema wa nchi jirani zinazozunguka Kigoma kwa kujenga ushuru wa forodha wa pamoja (One Stop Centre Border Post) ni kiwanda cha kuchakata zao la Mhogo ili kuepuka kuuza Malighafi.

Mhe. Dkt. Florence Samizi ameiomba Serikali kuongezewa bajeti ya TARURA ili kutengeneza Barabara zilizokatika katika Jimbo la Muhambwe ikiwemo Barabara ya Kigaga - Magarama - Kigoma na Barabara ya Kibondo Mjini - Murungu

Mhe. Dkt. Florence Samizi ameongeza kuwa kwa kufanya hivyo itasaidia kupunguza adha ya watu ambao ni Wanafunzi, Wajawazito na Wakulima kwenye changamoto ya usafiri.

WhatsApp Image 2024-07-13 at 15.47.28.jpeg
WhatsApp Image 2024-07-13 at 15.47.29.jpeg
WhatsApp Image 2024-07-13 at 15.47.29(1).jpeg
 
Hayo alitakiwa ayaseme bungeni.Pili Siyo Kazi ya serikali Kujenga viwanda.Viwanda vinajengwa na sekta binafsi.
 
Back
Top Bottom