Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
MHE. Edward Ole Lekaita Akichangia Bajeti ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Ofisi ya Rais TAMISEMI ya Tsh. Trilioni 10.125 Kwa Mwaka wa Fedha 2024/2025
"Namshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa heshima kubwa aliyotupa majimbo kupitia miradi ya maendeleo. Jimbo la Kiteto tumepata shule mpya za Sekondari tatu, madarasa 57 ya shule shikizi 18, VETA, Ambulance 🚑, magari 2, Vituo vya Afya na miradi mingi" - Mhe. Edward Ole Lekaita, Mbunge wa Jimbo la Kiteto
"Bungeni Mwaka 2021-2022 tulikubaliana tumalizane na Vituo vya afya vya Tarafa kabla ya kwenda kwenye Kata. Mpaka sasa Kiteto tunadai Vituo vya Afya vya Tarafa 3; Tarafa ya Makame, Kibaya na Dosidosi. Tulileta maombi ya Vituo vya kimkakati vya Matui na Dongo. Naombeni TAMISEMI tumalizane kwanza na Vituo vya afya kwenye Tarafa ndiyo twende wote kwenye Kata" - Mhe. Edward Ole Lekaita, Mbunge wa Jimbo la Kiteto
"Jimbo la Kiteto ni kubwa sana (linalingana na baadhi ya Mikoa) na mtandao wa barabara ni mkubwa karibu KM 1291 lakini tunapata bajeti ya Shilingi Bilioni 2.8 na uhalisia tulitakiwa tupate zaidi ya Shilingi Bilioni 11 lakini sisi tunataka nyongeza tu ya Shilingi Bilioni 5 tutaweza kuhangaika na barabara" - Mhe. Edward Ole Lekaita, Mbunge wa Jimbo la Kiteto
"Mvua zinazonyesha, Kiteto miundombinu imeharibika sana, hakuna mawasiliano kati ya Tanga na Kiteto maana barabara ni mbovu sana. Tunaomba Kiteto mtupe kipaumbele" - Mhe. Edward Ole Lekaita, Mbunge wa Jimbo la Kiteto
"Tunashukuru mmetupa Shilingi Milioni 900 kwaajili ya Hospitali za Wilaya kongwe lakini Wilaya ya Kiteto ni kubwa Imezungukwa na Wilaya saba. Bado upungufu wa miundombinu, Tunaomba TAMISEMI muangalie, Kiteto bado tuna uhitaji wa jengo la dharura (Emergency Medical Department), ICU, Reproductive Care Health (RCH), X-Ray ili Hospitali ya Wilaya ikamilike" - Mhe. Edward Ole Lekaita, Mbunge wa Jimbo la Kiteto
"Kiteto kuna miradi ya wananchi ambayo ni mabweni, Zahanati, madarasa. Wananchi wamejenga kwa nguvu zao wenyewe mpaka kufikia renta. Tunaomba TAMISEMI mtafute fedha Maalum ambayo kazi yake ni kuhangaika na miradi ya wananchi. Mbigili wana Zahanati yao, Magungu wamejenga bweni na Krashi, Zambia, Ilala." - Mhe. Edward Ole Lekaita, Mbunge wa Jimbo la Kiteto
"Asilimia 10 ya fedha za Halmashauri, mmetengeneza fomula ya kuanza na Halmashauri 10 na Sheria itabadirika. Ni vyema tufahamu kama suala linaanza mwezi Julai 2024 basi Sheria na kanuni zinazohitajika zikamilike mapema ili wananchi wasiendelee kuchelewa kusubiri mabadiliko ya Sheria" - Mhe. Edward Ole Lekaita, Mbunge wa Jimbo la Kiteto
"Kiteto ina shule 2 tu za kidato cha tano na sita. Tulishatuma maombi TAMISEMI na timu ikatumwa kuangalia shule za Ndido, Dongo, Njoro, Dosidosi na Sunya. Tunaomba majibu lini shule hizi zitapandishwa hadhi na kuwa na kidato cha tano na sita. Kiteto kuwa na shule 2 za kidato cha tano na sita siyo sawa" - Mhe. Edward Ole Lekaita, Mbunge wa Jimbo la Kiteto
"Kiteto nina Kata 2 hazina shule ya Sekondari, Kata ya Makame na Leseri. Nashukuru kwa tatu mlizotupa lakini Sera ya nchi ni kila Kata iwe na Sekondari. Ni vyema mkatupa kipaumbele tukapata shule 2 mpya za Sekondari ili tumalizane na Kata" - Mhe. Edward Ole Lekaita, Mbunge wa Jimbo la Kiteto