Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
Mbunge wa Lupembe, Edwin Swalle ameishauri Serikali kupunguza gharama za leseni ya madereva wa pikipki (bodaboda) kutoka elfu 70 za sasa hadi elfu 20.
Swalle amesema gharama hiyo ikipungua itawawezesha wengi kukata leseni na hivyo kupunguza hofu kwa madereva hao ambao wengi wao wakiona polisi wanawakimbia na mara nyingine kusababisha ajali na vifo.
Unaonaje wazo la mheshimiwa mbunge? Lakini kumbuka pia hatua yoyote ya kupunguza gharama za leseni ni kupunguza pia mapato ya serikali!