Mbunge wa Buchosa, Eric Shigongo, ameongoza maandamano ya amani kumuunga mkono Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kwa namna anavyotekeleza Ilani ya CCM kwa vitendo.
Katika maandamano hayo, pia kulifanyika zoezi la usimikaji wa bendera kwa mabalozi wa mashina pamoja na ukaguzi wa ujenzi wa shule mpya ya sekondari Chema, ikiwa ni sehemu ya miradi ya maendeleo inayoendelea kutekelezwa ndani ya jimbo hilo kupitia Serikali ya Awamu ya Sita.