Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
Esther Malleko atoa simu janja saba (milioni 2.1) kwa UWT Wilaya zote za mkoa wa Kilimanjaro kwaajili ya kusajili Wanawake kielektroniki
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Kilimanjaro, Mhe. Esther Edwin Malleko ametoa Simu Janja Saba (Smartphone 7) zenye thamani ya Shilingi Milioni 2.1 kwaajili ya usajili wa Wanachama wa UWT katika mfumo wa Kielektroniki.
Mhe. Esther Edwin Malleko ameyafanya hayo Mnamo tarehe 30 Aprili 2024 na kuwakonga nyoyo viongozi na Watendaji wa UWT Mkoa wa Kilimanjaro baada ya kutekeleza maelekezo ya UWT ya kuongeza wanachama wengi wapya wa jumuiya hiyo.
Soma Pia:
- Mbunge Norah Mzeru agawa simu janja (Smartphone) kwa UWT Wilaya ya Kilosa ili kusaidia kusajili Wanawake katika Mfumo wa Kielektroniki
- Mbunge Aysharose Mattembe Agawa Simu Janja 7 (4,500,00) kwa Wilaya za Mkoa wa Singida
Pamoja na hayo Mhe. Esther Mallek amefanya hivyo kutekeleza maagizo yaliyotolewa na viongozi wa UWT Taifa kupitia semina Mbalimbali zilizotolewa kwa Makatibu wa Mikoa na Wilaya, Wenyeviti, Wabaraza na Wajumbe wa NEC kupitia jumuiya ya UWT.
Aidha, Esther Malleko amekabidhi simu hizo kwa Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Kilimanjaro, Ndugu Elizabeth Minde na Katibu wa Katibu wa CCM Mkoa huo, Ndugu Mercy Malambo (MNEC)
Mwisho, Viongozi wa Chama Cha Mapinduzi na Jumuiya ya UWT Mkoa wa Kilimanjaro wamempongeza sana Mbunge Malleko kwa moyo wa kujitolea wa kuimarisha Jumuiya ya UWT kwa kutoa simu za kusajili kielektroniki wanachama wapya wa jumuiya hiyo.
KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI