Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
MBUNGE ESTHER MALLEKO AZUNGUMZA NA WANAWAKE WA MOSHI MJINI
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Kilimanjaro, Mhe. Esther Edwin Malleko tarehe 26 Julai, 2024 amefanya Ziara katika Wilaya ya Moshi Mjini na Kuzungumza na Wanawake kwa lengo la Kuimarisha Jumuiya ya UWT.
Mhe. Esther Malleko akiwa katika Tarafa ya Moshi Magharibi, Kata ya Longuo 'B' Manispaa ya Moshi Mjini alisisitiza Wanawake Wajitokeze na Washiriki ipasavyo Kujiandikisha katika Daftari la Kudumu la Mpiga Kura na pia wagombee nafasi katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa Unaotarajiwa Kufanyika mwaka 2024.
Mhe. Esther Malleko amesema kuwa ili kuwa mpiga kura halali katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa ni lazima kuwa na sifa ya kujiandikisha, hivyo ametoa rai kwa Wanawake kujiandikisha kwa wingi ili kuwa na uwakilishi wa Wanawake katika nafasi mbalimbali za uongozi nchini
Aidha, Mbunge Esther Edwin Malleko amewaeleza Wanawake wa Moshi Mjini mambo makubwa yaliyofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan na kuzidi kusisitiza Wanawake kumuunga mkono Rais kwa kazi nzuri anayoifanya nchini.
Vilevile, Mbunge Malleko amesisitiza Wanawake wa Moshi Mjini kuendelea kujisajiri katika Mfumo wa Kielektroniki wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na UWT ili kupata wanachama wapya wa CCM na UWT kwaajili ya kupiga kura za kishindo kwa Rais Samia Suluhu Hassan katika Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025.