Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
MBUNGE MHE. EZRA CHIWELESA ACHAGULIWA KUWA RAIS WA MOJA YA KAMATI BUNGE LA MAZIWA MAKUU.
Tarehe 27 Machi, 2023 umefanyika uchaguzi wa viongozi mbalimbali wa Kamati za Kudumu za Bunge la Nchi za Maziwa Makuu Jijini Juba Sudani Kusini.
Katika uchaguzi huo Mbunge wa Jimbo la Biharamulo Magharibi na kiongozi wa msafara wa Wabunge kutoka Tanzania Mhe. Eng. Ezra Chiwelesa amechaguliwa kuwa Rais wa kamati ya kudumu ya masuala ya kibinadamu na kijamii (Humanitarian and Social Issues).
Aidha, Jamhuri ya Afrika ya Kati wamechaguliwa kuwa Makamu wa Rais na Burundi wakichaguliwa kwenye nafasi ya katibu wa kamati.
Kuchaguliwa kwa Mhe. Ezra Chiwelesa kutoka Bunge la Tanzania kunadhihirisha kuaminika kwa Tanzania kimataifa hali iliyosababishwa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye ameimarisha masuala ya kidiplomasia.