Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
DKT. FLORENCE SAMIZI AGAWA MITUNGI YA GESI 200 KWA MAAFISA UPISHI 200 MUHAMBWE.
Mbunge wa Jimbo la Muhambwe, Mhe. Dkt. Florence George Samizi amehamasisha wananchi kushiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 27 Novemba, 2024.
Katika kuuunga mkono kazi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan anayepambana kupunguza uchafuzi wa mazingira na kuenenda na Mpango wa Taifa wa utunzaji wa mazingira kwa kutumia Nishati Safi ya Kupikia, Mbunge wa Jimbo la Muhambwe mkoani Kigoma Mhe. Dkt. Florence George Samizi ameweza kugawa takribani mitungi ya gesi 200 kwa Mama na Baba lishe.
Hii ni sehemu ya uungwaji mkono wa kampeni ya Taifa chini Rais Samia Suluhu Hassan ambapo zipo faida chanya nyingi za utumiaji wa Nishati Safi ya Kupikia ukilinganisha na utumiaji wa kuni na mkaa.
Utumiaji wa Nishati Safi ya Kupikia kama gesi hupunguza uzalishaji wa Gesi ya ukaa ambayo ni mbaya kiafya, kuokoa misitu, kulinda afya kwani majiko yanayotumia nishati safi hupunguza moshi hatari unaotokana na kuni
Attachments
-
WhatsApp Image 2024-10-01 at 08.36.08.jpeg83.2 KB · Views: 4 -
WhatsApp Image 2024-10-01 at 08.30.24.jpeg70.6 KB · Views: 3 -
WhatsApp Image 2024-10-01 at 08.30.24(1).jpeg90.4 KB · Views: 3 -
WhatsApp Image 2024-10-01 at 08.30.23.jpeg84.6 KB · Views: 2 -
WhatsApp Image 2024-10-01 at 08.30.23(1).jpeg79.9 KB · Views: 3 -
WhatsApp Image 2024-10-01 at 08.30.23(2).jpeg94.4 KB · Views: 3 -
WhatsApp Image 2024-10-01 at 08.30.22.jpeg91.5 KB · Views: 3 -
WhatsApp Image 2024-10-01 at 08.30.22(1).jpeg83.2 KB · Views: 2