Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
MBUNGE MHE. HUSNA SEKIBOKO AGAWA MITUNGI YA GESI KIJIJI CHA LUKOZI, LUSHOTO-TANGA
Mbunge wa Viti Maalum CCM Mkoa wa Tanga, Mhe. Husna Juma Sekiboko tarehe 11 Machi, 2023 alifanya ziara katika kijiji alichozaliwa, Lukozi na kuzungumza na wananchi wa kijiji hicho ambao walimueleza Mbunge changamoto ya Elimu.
Mhe. Sekiboko ameandika; "Nimepata fursa ya kufanya mkutano nyumbani katika Kijiji nilipozaliwa. Asanteni sana watu wa Lukozi, kwa hakika mmeupiga mwingi sana, mmenitia moyo sana, mmenipa nguvu na ari zaidi"
"Katika mkutano wetu tumepata bahati ya kuungwa mkono na ndugu zetu wa Taifa Gas na tumegawa majiko ya gesi kutoka Taifa Gas kwa akina Mama wajasiriamali wa Chakula (Mama lishe). Kwa pamoja tujenge uchumi wetu Asante sana Taifa Gas"
Itakumbukwa kuwa Mnamo tarehe 08.08.2023, Taifa Gas Tanzania Limited ilishirikiana na Mhe. Husna Sekiboko na kugawa mitungi 100 bure kabisa kwa wajasiriamali wa Lukozi kwa ajili ya kupata nishati safi ya kupikia kutoka Taifa Gas Tanzania
Aidha, katika hatua nyingine katika Maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani wilayani Lushoto Mhe. Husna Sekiboko ndiye aliyekuwa mgeni rasmi akishirikiana na viongozi wa Chama na Serikali akiwemo Mkuu wa Wilaya ya Lushoto Mhe. Kalisti Lazaro.