Sijali
JF-Expert Member
- Sep 30, 2010
- 2,672
- 1,814
Ni dhahiri kabisa, kutokana na michango yake bungeni, mbunge Msukuma anawashinda wengi kwa maono na ubunifu.
Amekuwa consistent kutoa maoni yenye mashiko, yaliyofanyiwa utafiti na hata kuthubutu kuonesha tija ya maoni yake endapo yatatumika. Hizi kwa kawaida ni sifa za mtu aliyebobea katika 'usomi'.
Ila kitu ninachohitalifiana naye ni ile ada yake ya mara kwa mara ya kuwabehua wasomi; kiasi kwamba ameanza kuwaaminisha vijana wavivu kuwa kusoma 'si lazima' na kwamba mtu anaweza kufika mbali kwa ujanja ujanja tu, bila ya kusoma!
Rai hii imeanza kushika mizizi sana baina ya makundi ya vijana Tanzania. Vijana wengi ninaozungumza nao wanaamini kuwa elimu si muhimu kwa mafanikio.
Sisemi kuwa Msukuma pekee ndiye anayehusika na hili, lakini nahofia kiasi anavyoendelea kulishabikia hilo, tena kutoka kilele cha taasisi ya uongozi, kitazidisha hisia hiyo.
Ukweli ni kuwa elimu ni muhimu sana kwa maendeleo ya mtu binafsi na taifa, na bila ya elimu si mtu wala taifa litafika popote.
Hii si kusema hakutakuwepo watu wachache, kama bwana Msukuma, ambao watakuwa na talanta au kipawa cha maarifa nje ya mfumo wa elimu. Lakini hii ni 'phenomenon' si sheria. Kosa ni kuifanya hii ni sheria na si 'phenomenon'.
Aidha, hao 'wasomi' ambao bwana Msukuma anawabehua, kwa kweli wengi wao hawakuelimika. Kuna tofauti kubwa baina ya 'kwenda Shule' na kuelimika. 'Usomi' au kuelimika kunaweza kutokea bila ya kwenda shule.
Wengi wanaoitwa 'wasomi' hapa Tanzania, kwa kweli wamekwenda shule tu, hawakuelimika!