Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
MBUNGE JACQUELINE KAINJA NA WANAWAKE (UWT) WILAYA YA KALIUA
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Tabora, Mhe. Jacqueline Kainja Andrew tarehe 13 Julai, 2023 ameendelea na zoezi la Ugawaji wa fedha za miradi ambapo amefanikiwa kukutana na kuwakabidhi Wajumbe Wote wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) kutoka Kata 28 zilizopo Wilayani Kaliua
Mhe. Jacqueline Kainja amesema kuwa miradi ya UWT Wilaya ya Kaliua inatofautiana na haifanani kutokana na uhitaji wa Kata husika kwani ilichaguliwa na Wajumbe wenyewe kwa kila Kata anazopita kuwawezesha wanawake kiuchumi.
Mhe. Jacqueline Kainja ametoa Elimu na semina kwa wanawake wa UWT Wilaya ya Kaliua juu ya miradi wanayoianzisha ili izae matunda kwani wabunge wanajinyima kuhakikisha akina Mama wanainuka kiuchumi
Mhe. Jacqueline Kainja amesisitiza wanawake kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan na kuwasisitiza akina Mama mwaka 2024 kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa wajitokeze wakagombee na kufuata nyayo za Rais Samia katika uongozi wa wanawake
Wanawake wa UWT Wilaya ya Kaliua wanajishughulisha na shughuli mbalimbali za kiuchumi ikiwemo Kilimo cha Michikichi, Uuzaji wa Samaki, Ufugaji wa Mbuzi, Uuzaji wa Vitenge na Uuzaji wa Sare za Chama Cha Mapinduzi (CCM na Jumuiya za UVCCM, UWT na Wazazi)