Pre GE2025 Mbunge Jafari Chege Aja na Mkakati Mpya Katika Kongamano la Vijana Rorya Tunaruka na Mama Samia 2025

Pre GE2025 Mbunge Jafari Chege Aja na Mkakati Mpya Katika Kongamano la Vijana Rorya Tunaruka na Mama Samia 2025

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301
Mbunge wa Jimbo la Rorya Mkoa wa Mara, Mhe. Jafari Wambura Chege ameandaa Kongamano la Vijana Rorya Tunaruka na Mama Samia lililohusisha Semina za mafunzo mbalimbali yenye fursa kwa Vijana wa Rorya.

"Leo ni siku ya Vijana Rorya bila kujali itikadi za Vyama vya Siasa. Natamani niwaone vijana mkiwa mmeungana nyote kama Vijana kwasababu ni siku ya Vijana wa Rorya" - Mhe. Jafari Wambura Chege, Mbunge wa Jimbo la Rorya

"Mimi ni Mbunge wenu na ni Mbunge kijana. Tunataka tuwaoneshe wana Rorya na wengine waliopo nje ya Rorya kwamba sisi Vijana tuko na Mama Samia Suluhu Hassan ambaye ametufanyia mambo mengi katika Jimbo la Rorya na mimi nitayasema vizuri yote yaliyofanywa"

"Ndugu zangu Vijana mkienda huko kwenye maeneo yenu muwaambie kuwa sisi Rorya kwa kazi iliyofanyika kwa miaka mitatu, kwa maendeleo yaliyofanyika na tumeona kwa macho yetu, sisi wana Rorya mwaka 2025 tunaruka na Mama Samia Suluhu Hassan"

"Watu wote nje ya Rorya wajue kuwa Vijana sisi hatuna kingine zaidi cha kumlipa Rais Samia Suluhu Hassan zaidi ya Kura nyingi sana za kutosha za kishindo mwaka 2025 na hatutaki mtu atuangushe. Muwaambie vijana wenzenu huko, Rorya hatuna baya na Mama Samia Suluhu Hassan. Lazima wana Rorya tutoe shukurani kama wana Rorya"

"Ni kweli mimi Mbunge ndiye ninayeomba miradi hii lakini bila Mama Samia Suluhu Hassan miradi isingefanyika. Mama hajawahi kufika Rorya lakini anamsikia Mbunge akiisemea Rorya na anapeleka fedha ili siku akija akute mengi yamefanyika na tunahitaji kuungana kuendelea kumsemea Mama".

WhatsApp Image 2024-08-10 at 18.48.23.jpeg
WhatsApp Image 2024-08-10 at 18.48.23(1).jpeg
WhatsApp Image 2024-08-10 at 18.48.24.jpeg
WhatsApp Image 2024-08-10 at 18.48.27.jpeg
WhatsApp Image 2024-08-10 at 18.46.50.jpeg
 
Back
Top Bottom