Mbunge Janejelly James Ntate afanya Ziara mkoa wa Dar es Salaam

Mbunge Janejelly James Ntate afanya Ziara mkoa wa Dar es Salaam

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Dar es Salaam Janejelly James Ntate amefanya ziara ya kikazi katika Mkoa wa Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya majukumu yake kama Mbunge wa Mkoa wa Dar es Salaam.
WhatsApp Image 2023-03-01 at 14.20.59(3).jpeg

Ntate alipata nafasi ya kuzungumza na watumishi wa Manispaa ya Jiji la Dar es Salaam ikiwa ni katika muendelezo wa ziara yake hapa jijini na katia kuelekea sherehe za kutimiza Miaka miwili ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan madarakani ambapo sherehe hizo zitafanyika tarehe 19 Machi 2023.

Tarehe 24 Februari 2023 Ntate aliambatana na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Dar es Salaam Ndugu Abbas Zubeir Mtemvu; Abdullah Jafar Chaulembo, Mbunge wa Jimbo la Mbangala pamoja na Kamati ya Siasa ya Wilaya Temeke katika kukagua utekelezaji wa Ilani ya CCM kwenye Jimbo la Mbagala.
WhatsApp Image 2023-03-01 at 14.20.58.jpeg

Ntate katika muendelezo wa ziara yake jijini Dar es Salaam alikutana na watumishi wa Manispaa ya Ubungo ambapo wote kwa pamoja wameahidi kwenda kumpa nguvu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan katika sherehe za kutimiza miaka miwili madarakani.

Ntate, mnamo tarehe 21 Februari 2023 alikutana na watumishi wa Manispaa ya Kinondoni katika ukumbi wa Shule ya Sekondari Turiani. Katika mkutano huo, Mhe. Ntate ambaye ni Mbunge wa wafanyakazi Viti Maalum amesisitiza watumishi wote wa Manispaa ya Kinondoni kumuunga mkono Rais Samia katika sherehe za kukaa madarakani miaka miwili.

Ntate aliwasisitiza watumishi kuendelea kuwa na imani kubwa na Rais Samia kwani kulingana na utendaji wake mkubwa na utekelezaji wa miradi mingi ya maendeleo inayoendelea na iliyokamilika tayari.

Kwa upande wao watumishi wa Manispaa ya Kinondoni wamesema kuwa wapo tayari na kuahidi kuwa kuelekea sherehe za maadhimisho ya miaka miwili ya mama Samia watakuwepo.

Mapema tarehe 18 Februari 2023, Ntate alishiriki Mkutano wa Baraza la Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) katika Wilaya ya Temeke; Na, Tarehe 18 Februari 2023 alishiriki kikao Maalum na viongozi wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Taifa.

WhatsApp Image 2023-03-01 at 14.20.56.jpeg
 

Attachments

  • WhatsApp Image 2023-03-01 at 14.20.58(2).jpeg
    WhatsApp Image 2023-03-01 at 14.20.58(2).jpeg
    38.7 KB · Views: 1
  • WhatsApp Image 2023-03-01 at 14.20.59(2).jpeg
    WhatsApp Image 2023-03-01 at 14.20.59(2).jpeg
    57.7 KB · Views: 1
Wabunge wa koneksheni bhana ! hafamiki popote zaidi kwa yule aliyemteua ! noma sana !
 
Back
Top Bottom