Mbunge Jimbo la Lupembe, Edwin Swale: Bajeti ya Wizara ya Ujenzi haina matumaini kwa Watanzania

Mbunge Jimbo la Lupembe, Edwin Swale: Bajeti ya Wizara ya Ujenzi haina matumaini kwa Watanzania

beth

JF-Expert Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
3,880
Reaction score
6,368
Mbunge wa Jimbo la Lupembe, Edwin Swale amesema Bajeti wa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi imeanza vibaya na haina matumaini kwa Watanzania wengi, Wabunge wote wanalalamika na Waziri naye amekata tamaa.

Amesema Wananchi wa Lupembe wamekuwa wakifurika kwenye Kampeni na kushangilia ujio wa barabara ya Kibena mpaka Madeke na mwaka 2020 Wizara iliitengea Bilioni 5.9, lakini leo Wizara hiyo hiyo imepunguza fedha hadi Bilioni 2.

Ameongeza, "Waziri nisaidie kujua nini kimekusibu kuipunguza kutoka Bilioni 5 mpaka 2? Wananchi wa Lupembe tumekosa nini? Fedha hii umeiondoa umepeleka wapi na kwanini?"
 
Back
Top Bottom