stonecutter
JF-Expert Member
- Jun 12, 2022
- 1,724
- 2,584
Salam wakuu.
Niende kwenye mada. Katika kuzunguka huku na kule ndani ya nchi ktk kutimiza majukumu yangu, mwishoni mwa juma lililopita nilikuwa kusini mwa nchi. Mkoani Ruvuma, wilaya moja ya Nyasa ambayo makao yake makuu ni Mbamba Bay.
Sasa, kwa siku mbili mfululizo yaani Alhamisi na Ijumaa, kulikuwa na matangazo khs mkutano wa siku moja wa Gwajima siku ya Jumamosi. Matangazo ya mkutano yalieleza wazi kwamba, kutakuwa na kutoa misukule, yaani watu waliokufa kishirikina ndani ya ziwa Nyasa au penginepo.
Matangazo yalisema wazi kuwa, wale waliofiwa na wapendwa wao waje na picha zao na kuandika majina matatu ya aliyekufa. Wakuu, kule kusini dhana ya uchawi na watu kufa vifo vya utata wenyeji walisema imeshamiri sana.
Hivyo Gwajima alisubiriwa kwa shauku kubwa watu wakiwa na picha za wapendwa wao. Siku ikawadia, Gwajima akaanza kazi. Baada ya mahubiri machache akaanza kuita misukule, njoooo, njooo, hadi mwisho, hakuna hata msukule uliofika pale. Wenyeji wamelaumu udanganyifu uliofanyika. Gwajima hii dhambi tubuni.