Pre GE2025 Mbunge Juliana Masaburi ‘Awashika Mkono’ UVCCM Wilaya ya Ilala Ujenzi Nyumba ya Mtumishi

Pre GE2025 Mbunge Juliana Masaburi ‘Awashika Mkono’ UVCCM Wilaya ya Ilala Ujenzi Nyumba ya Mtumishi

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301

MBUNGE JULIANA MASABURI AWASHIKA MKONO UVCCM WILAYA YA ILALA UJENZI NYUMBA YA MTUMISHI

Mbunge wa Viti Maalum Vijana Taifa (Anayetokea Mkoa wa Mara) Mhe. Juliana Didas Masaburi tarehe 03 Agosti, 2024 alikuwa mgeni rasmi katika ufungaji wa Baraza la UVCCM Wilaya ya Ilala Mkoani Dar es Salaam ambapo aliambatana na Katibu wa UVCCM Mkoa wa Dar Es salaam, Ndugu Hussein Egobano.

Mhe. Juliana Masaburi akiwa katika Baraza la UVCCM Wilaya ya Ilala alichangia Simu Janja Mbili (Smartphone) kwaajili ya Kuwezesha na kuongeza kasi ya Usajili wa wanachama wapya CCM na UVCCM katika mfumo wa kielektroniki (TEHAMA) kwa Wilaya ya Ilala.

Akizungumza katika Baraza hilo, Mhe.Juliana Masaburi alisema kuwa amefanya hivyo ili kuunga mkono juhudi zinazofanywa na Mwenyekiti UVCCM Taifa, Ndugu Mohamed Kawaida kwa kuchangia Simu Janja Mbili ili Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Iendelee kuvuna Wanachama Wapya na Wanachama wengi watakaokiwezesha Chama Cha Mapinduzi kushinda kwa kishindo katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa wa Novemba 2024 na Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025.

Aidha, Juliana Masaburi alichangia fedha taslimu Shilingi Milioni Moja (Tsh. 1,000,000) na kuahidi kutoa kiasi kingine cha fedha cha Shilingi Laki Tano (500,000) kwaajili ya Kuwezesha ujenzi wa nyumba ya Katibu wa UVCCM Wilaya ya Ilala.

"Niwaombe ndugu zangu, uongozi wa UVCCM Wilaya ya Ilala na Wanachama tuongeze juhudi katika kusajili Wanachama wapya katika mfumo wa kielektroniki na lengo ni kuhakikisha tunapata Kura nyingi sana za kutosha za Mheshimiwa Rais wetu Mpendwa Dkt. Samia suluhu Hassan ifikapo mwaka 2025" - Mhe. Juliana Masaburi, Mbunge wa Viti Maalum (Vijana Taifa)

Akisisitiza watu kujitokeza kujiandikisha kwenye Daftari la Kudumu la Mpiga Kura, Mbunge Masaburi alisema kuwa "Ninatamani tusajili wanachama wengi kuelekea uchaguzi wa Serikali za Mitaa wa Novemba 2024 na Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025"
Soma pia: Mbunge Christina Mnzava Agawa Vifaa vya Michezo kwa Wanafunzi Shinyanga Vijijini

WhatsApp Image 2024-08-03 at 23.24.07(1).jpeg
WhatsApp Image 2024-08-04 at 10.27.35(1).jpeg

WhatsApp Image 2024-08-03 at 23.24.08.jpeg
 

Attachments

  • WhatsApp Image 2024-08-03 at 23.24.07(1).jpeg
    WhatsApp Image 2024-08-03 at 23.24.07(1).jpeg
    472.8 KB · Views: 6
Back
Top Bottom