Pre GE2025 Mbunge Juliana Shonza Akabidhi Mifuko ya Saruji 20 (400,000) Ujenzi Ofisi za UWT Kata

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Songwe, Mhe. Juliana Daniel Shonza amefanya Ziara ya Kata kwa Kata huku akipokelewa kwa shangwe na wananchi wa Kata ya Harungu iliyopo Wilaya ya Mbozi Mkoani Songwe.​

Akiwa katika Kata ya Harungu, Mhe. Juliana Daniel Shonza amekabidhi mifuko ya Saruji 20 yenye thamani ya Shilingi Laki Nne (400,000) kwaajili ya Ujenzi wa Ofisi ya Jumuiya ya Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) ya Kata ya Harungu.

Mhe. Juliana Daniel Shonza ameelezea Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM 2020-2025; Kuzungumza na Wanawake kuhusu utolewaji wa mikopo ya Asilimia Kumi (10%); Kuwezesha Wanawake Wajasiriamali Kiuchumi; Kuendesha Kampeni ya Kupinga Ukatili na Unyanyasaji wa Kijinsia; Kuendesha Kampeni ya Kupinga Mimba za Utotoni; Kampeni ya Kuhamasisha Lishe Bora kwa Mama na Mtoto.

Mhe. Juliana Daniel Shonza amesisitiza sana Wananchi wote wa Kata ya Harungu kujitokeza kwa wingi Kujiandikisha katika Daftari la Kudumu la Mpiga Kura ili wapate haki ya kupiga kura wakati wa uchaguzi.

Mwisho, Mhe. Juliana Daniel Shonza amewasihi wananchi wote na viongozi kuendelea kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kazi nzuri sana aliyofanya nchini ikiwemo Mkoa wa Songwe.
 
Uwt ofisi...ndo kachangia..tena laki 4!!! Imekuwa habari! Na picha lukuki!!! Hongereni kwa mtakao nufaika na ujenzi huo...
 
Zile nyakati pendwa zimekaribia sasa, jana yule profesa feki wa Ubungo aliyewekwa na Yohana alikua pale Mabibo akawaahidi Bodaboda kuwapatia ardhi, yaani Bodaboda apewe ardhi.....Mkumbo buana
 
Mbona hapa kwetu Tanga mifuko ni elfu 14 Kwa 15, kwahio mifuko 20 gharama ni laki 3.
 
Mifuko 20 ndiyo debe lote hili !! Kwa wale wasiomjua Lucas Mwashambwa ni huyo kulia kwa Shonza aliyevaa shati la kaki na suruali ya blue. ephen_ unamuona bebi wako alivyotokelezea mchicha hapo?
 
Hiyo kwenye mabano (400,000)ni nini!!??
 
Hafla ya kupokea hiyo mifuko inaweza ikawa imegharimu pesa nyingi kuliko cement yenyewe
 
Mifuko 20 ndiyo debe lote hili !! Kwa wale wasiomjua Lucas Mwashambwa ni huyo kulia kwa Shonza aliyevaa shati la kaki na suruali ya blue. ephen_ unamuona bebi wako alivyotokelezea mchicha hapo?
Hahahaha sure mkuu ni yeye.
 
Siyo shule?!
Angalia nyuma nyumba za ki MASKINI ZINAVYOTISHA!
Uzombie, ujinga, ufukara, elimu, uzuzu wetu unawafanya hawa kufanya ujinga ujinga usio NA KIFANI!
KWANINI SIYO SHULE, ZAHANATI, LIBRARY.....
🤬🤬🤬🤬
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…