Mbunge Juliana Shonza Awapiga Marufuku Wanaotapeli Wajane Wilaya ya Mbozi

Mbunge Juliana Shonza Awapiga Marufuku Wanaotapeli Wajane Wilaya ya Mbozi

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301

MBUNGE JULIANA SHONZA AWAPIGA MARUFUKU WANAOTAPELI WAJANE WILAYA YA MBOZI

"Wanaibuka watu, badala ya kuwasaidia na kuwaunganisha wajane wao wanafanya kuwatapeli na kuwafilisi wajane. Nilipolisikia hilo nimelifuatilia sana, niliwasiliana na viongozi wanaohusika na Masuala ya wajane Wizarani. Chama Cha Umoja wa Wajane kuanzishwa kwenye Wilaya ya Mbozi Mkoa wa Songwe siyo jambo baya" - Mhe. Juliana Daniel Shonza, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Songwe

"Kuanzishwa kwa Chama Cha Umoja wa Wajane Wilaya ya Mbozi (Songwe) siyo jambo baya. Jambo baya ni namna ya uendeshaji wa hicho Chama unavyofanyika. Mnakusanya kwa wabibi wa Ichenjenzya wenye miaka 60 na miaka 70 mnawaambia watoe 10,000 ili Rais Samia aje awape fedha" - Mhe. Juliana Daniel Shonza, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Songwe

"Kuwachangisha fedha Wajane kwamba Rais Samia atakuja kuwapa fedha ni kumchonganisha Rais Samia na wanawake wa Mbozi. Jambo hilo hatutalikubali kwasababu kitu hicho hakipo. Kama ni fedha Rais Samia ameshazitoa tunazo asilimia 10 lakini siyo kukusanya fedha za Wajane kuwaambia njooni Mbeya Mama Samia anakuja" - Mhe. Juliana Daniel Shonza, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Songwe

"Mnakusanya 5,000 Ichenjenzya mnawaambia baada ya Miaka 3 tutawapa fedha bila riba. Mnachukua vitenge kwa 7,000 Tunduma mnawauzia Wajane kwa 15,000. Mbaya zaidi mnawaambia njoni Mbeya Mama Samia anakuja kuwapa fedha" - Mhe. Juliana Daniel Shonza, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Songwe

"Mimi niwaonye. Uongozi upo, Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti, Katibu na Mweka Hazina yupo. Niwaombe wale viongozi wote waliohusika kwenye kuwarubuni na kuwalaghai wanawake na kuwafungulia akaunti za benki hewa moja kwa moja wasimamishwe nafasi zao kuanzia leo siyo viongozi" - Mhe. Juliana Daniel Shonza, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Songwe

"Tunacho Chuo cha DIT, mwaka huu wa fedha tumeletewa Chuo cha VETA cha Mkoa wa Songwe kinajengwa ndani ya Mkoa wa Songwe. Rais alipoingia madarakani alikuta kidato cha kwanza mpaka cha nne hakuna ada, akasema hapana aongeza mpaka kidato cha sita hakuna ada" - Mhe. Juliana Daniel Shonza, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Songwe

"Rais Samia hataki kuona mtoto anakosa haki yake ya Msingi ya kupata Elimu kwasababu mzazi wake hawezi kumsomesha. Niwaombe Ndugu zangu wa Mbozi na Vwawa tusimamie kuhakikisha watoto wetu wanasoma. Bajeti ya fedha mwaka 2023-2024 amesema anafuta ada kwenye Vyuo vya Kati" - Mhe. Juliana Daniel Shonza, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Songwe

WhatsApp Image 2023-07-15 at 06.47.13.jpeg
 
Back
Top Bottom