upupu255
Senior Member
- Sep 4, 2024
- 119
- 144
Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Patrobas Katambi, ambaye pia ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu,Kazi,Ajira,Vijana na watu wenye ulemavu,ameshiriki na wananchi ujenzi wa msingi wa Zahanati ya Ibanzamata,pamoja na kuchangia Sh.milioni 10.
Ameshiriki ujenzi wa msingi huo leo akiwa ameambatana na viongozi mbalimbali wa chama,wakiongozwa na Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Shinyanga Mjini Anord Makombe.
Kupata taarifa na matukio yanayojiri kuelekea uchaguzi mkuu kwa kila mkoa ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025
Amewapongeza wananchi wa Ibinzamata kwa kujitoa katika masuala ya maendeleo,hivyo ameamua kushirikiana nao kwenye ujenzi wa Zahanati hiyo,na kwamba atahakikisha inakamilika na kuanza kutoa huduma.
"Nimefurahishwa na nyie wananchi kwa kujitoa katika masuala ya maendeleo juu ya ujenzi wa Zahanati hii, na mimi nitachangia Sh.milioni 10 na tutashirikiana hadi kufikia hatua ya lenta na baada ya hapo tutatafuta fedha ili kuikamilisha kabisa," amesema Katambi.