Pre GE2025 Mbunge Kimei achangia shilingi milioni tano ujenzi wa Madrasa Msikiti mkuu wa Taqwa - BAKWATA Kahe

Pre GE2025 Mbunge Kimei achangia shilingi milioni tano ujenzi wa Madrasa Msikiti mkuu wa Taqwa - BAKWATA Kahe

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

MTANZANIA620

Member
Joined
Jun 20, 2023
Posts
65
Reaction score
81
IMG_20240830_143958_988.jpg
Mbunge wa Jimbo la Vunjo Mheshimiwa Dkt Charles Stephen Kimei ameendelea kuunga mkono juhudi za madhehebu ya dini katika kujenga miundombinu mbalimbali yenye lengo la kutoa huduma za kiimani na kujenga maadili kwa jamii.

Katika kuhakikisha hilo jana tarehe 30 Agosti, 2024 ametekeleza ahadi yake ya shilingi milioni tano yenye lengo la kuwaunga mkono waumini wa imani ya Kiislamu Msikiti mkuu wa Taqwa BAKWATA kata ya Kahe walioamua kujenga vyumba viwili vya elimu ya awali pamoja Madrasa kwa kujitolea wao wenyewe kwa hali na mali pamoja na kushirikisha wadau mbalimbali.

Soma Pia: Kimei aendelea kuweka rekodi Vunjo

Uongozi wa msikiti huo pamoja na BAKWATA kata ya Kahe wamemshukuru Dkt Kimei kwa mchango wake na kumpongeza kwa kutowabagua wananchi anaowawakilisha kwa imani zao.

Dkt Kimei amewaomba viongozi wote wa dini kuendelea kuiombea Tanzania na kumuombea Mheshimiwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan ili aendelee kuiongoza Nchi yetu katika usawa na haki.
 
Mbunge wa Jimbo la Vunjo Mheshimiwa Dkt Charles Stephen Kimei ameendelea kuunga mkono juhudi za madhehebu ya dini katika kujenga miundombinu mbalimbali yenye lengo la kutoa huduma za kiimani na kujenga maadili kwa jamii.

Katika kuhakikisha hilo jana tarehe 30 Agosti, 2024 ametekeleza ahadi yake ya shilingi milioni tano yenye lengo la kuwaunga mkono waumini wa imani ya kiislamu msikiti mkuu wa Taqwa Bakwata kata ya Kahe walioamua kujenga vyumba viwili vya elimu ya awali pamoja madrasa kwa kujitolea wao wenyewe kwa hali na mali pamoja na kushirikisha wadau mbalimbali.

Uongozi wa msikiti huo pamoja na BAKWATA kata ya Kahe wamemshukuru Dkt Kimei kwa mchango wake na kumpongeza kwa kutowabagua wananchi anaowawakilisha kwa imani zao.

Dkt Kimei amewaomba viongozi wote wa dini kuendelea kuiombea Tanzania na kumuombea Mheshimiwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan ili aendelee kuiongoza Nchi yetu katika usawa na haki.
ANAJISUMBUA HAONI NDANI
 
Back
Top Bottom