Mbunge Kingu: Serikali irudisheni SONGAS

Mbunge Kingu: Serikali irudisheni SONGAS

Mnada wa Mhunze

Senior Member
Joined
Mar 1, 2023
Posts
168
Reaction score
819
Mbunge wa Singida Kusini Elibariki Kingu ameitaka Serikali iipe mkataba mnono tena kampuni ya Songas ili iendelee kuiuzia Serikali umeme

Ameyasema leo bungeni Dodoma
 
mkataba mnono tena kampuni ya Songas ili iendelee kuiuzia Serikali umeme

TOKA MAKTABA

04 August 2022

KESHO YA MRADI WA GESI YA SONGOSONGO

PANAFRICAN ENERGY Managing Director, Andrew Hanna MBE highlights the status of PanAfrican Energy Tanzania's Natural Gas Exploration and the foreseeable future
4 August 2022
Mkurugenzi wa PANAFRICAN ENERGY Bw. Andrew (Andy) Hanna azungumzia changamoto na mipango endelevu ya mradi wa gesi wa Songosongo kwa kina kabisa kwa kuangalia mwaka 2026....

Mradi wa SONGAS unaosafirisha gesi kwa bomba hadi Dar es Salaam kutoka mitambo katika kisiwa cha Songosongo field una changamoto za uchakavu, mitambo kupata kutu na kuonesha uhalisia wake ambao miaka 30 iliyopita haijufahamika.

Hivyo kuhitaji utafiti wa kina kujua kama kutaanza kuwepo upungufu wa uzalishaji wa gesi ya Songosongo au la kwani kunadalili kisima kupunguza mbinyo (pressure) hivyo kuna hatihati je nini hasa kifanyike kuhakikisha gesi inazalishwa kwa kiwango hitajika hadi mwezi Oktoba 2026 ...

Source : The Guardian Digital
 
Kama Songas wapo tayari iuzia umeme Tanzania chini ya Tsh 250 kwa unit moja sioni shida kwa wao kuendelea kuzalisha umeme kwa matumizi yetu. Maana bado Tanesco wenyewe kuna maeneo mengine wanazalisha umeme kwa gharama ya TSH 700 au zaidi na kuwauzia wananchi kwa TSH 350.
 
Kama Songas wapo tayari iuzia umeme Tanzania chini ya Tsh 250 kwa unit moja sioni shida kwa wao kuendelea kuzalisha umeme kwa matumizi yetu. Maana bado Tanesco wenyewe kuna maeneo mengine wanazalisha umeme kwa gharama ya TSH 700 au zaidi na kuwauzia wananchi kwa TSH 350.
Shida haionekani sasa, Ila baada ya muda huwa wanafanya lobbying kwa viongozi alafu mnaletewa hadithi za gharama za uzalishaji zimepanda duniani hivyo umeme pia unapanda
 
Back
Top Bottom