Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,060
- 5,648
Mbunge Jumanne Kishimba, ambaye ni mjumbe wa Kamati ya Elimu ya Juu, ametoa maoni yake Bungeni kuhusu hali ya mikopo ya elimu nchini. Maoni hayo yalikuja baada ya Bodi ya Mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu (HESLB) kudai kushindwa kupata marejesho kutoka kwa waliokopa mikopo ya elimu na kutangaza kuandaa oparesheni ya kuwakamata wadaiwa wote. Kishimba alisisitiza kuwa Bodi ya Mikopo inapaswa kuwajibikaji zaidi katika kutoa mikopo kwa wanafunzi. "Bodi ya Elimu imempa mtu wa chuo hizo pesa, mtu wa chuo akampa Elimu mwanafunzi, elimu ambayo haiajiriki. Sasa anayetakiwa kushitakiwa ni nani? Ni mwanafunzi au ni Chuo?" alihoji Kishimba.
Pia, Soma: Bodi ya mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu HESLB imetimiza miaka 20, je imekuwa msaada ipavyo kwa wanafunzi wasiokuwa na uwezo kufikia elimu ya juu?
Mbunge huyo aliongeza kuwa, kwa sasa, dunia inabadilika na kwamba hatuwezi kuendelea kutumia kauli za kale kama "Elimu ni Ufunguo wa Maisha," wakati wanafunzi wanapewa bidhaa ambayo hawana uwezo wa kuiuza. Aliiomba Bodi ya Mikopo kuongeza masharti kwa vyuo ili kuhimiza utoaji wa elimu inayohakikisha ajira kwa wahitimu. "Kama Bodi ya Mikopo inazitupa tu hela kwa mtu halafu anaenda kumfundisha GPA isiyoajirika, taasisi hii si itafilisika," alisisitiza.
Aidha, Kishimba alitoa wito kwa taasisi za elimu (Vyuo) kutafuta mitaala inayolenga kuwapa wanafunzi ujuzi unaohitajika kwenye soko la ajira, ili waweze kurejesha mikopo yao kwa ufanisi.