ChoiceVariable
JF-Expert Member
- May 23, 2017
- 66,537
- 75,687
Rais Samia ameendelea kuingia kwenye nyoyo za Watanzania hususani Wana Iringa baada ya kutoa Fedha za kuanza Ujenzi wa Barabara ya Iringa-National Park ambayo ilikuwa ni Kilio kikubwa Cha wana Iringa.
Ameyasema hayo Leo hii baada ya kushuhudia utiaji Saini wa mkataba wa kuanza ujenzi wa Barabara hiyo yenye urefu wa km 104 Kwa kiwango cha Lami.
=============
My Take
Rais Samia amedhamiria kuifungua Mkoa wa Iringa.
1. Ujenzi wa Barabara ya Iringa-Kilolo-Ifakara unaendelea
2. Ujenzi wa Barabara ya Iringa Bypass(Kihesa-Iringa Bus Terminal)
3. Ujenzi wa Barabara ya Mafinga-Mgololo
4. Ujenzi wa Barabara ya Iringa-Msembe
5. Upanuzi wa Barabara ya Tanzam(mlima Kitonga).
Hapo ni miradi ya Barabara tuu Bado sekta zingine.Kuna mgombea yeyote ataweza kumsemea shit Rais Samia?
Samia Anatosha na chenji inabaki.
Kazi imeanza 👇👇
==========
MKATABA UJENZI WA BARABARA YA IRINGA - MSEMBE WASAINIWA, BILIONI 142.5 KUTUMIKA
Serikali imesaini mkataba wa ujenzi wa barabara ya Iringa - Msembe inayoelekea kwenye Hifadhi ya Taifa ya Ruaha (km 104) kwa kiwango cha lami utakaogharimu kiasi cha shilingi Bilioni 142.56 ili kufungua fursa za kiutalii, kiuchumi na kibiashara kwa mikoa ya Nyanda za Juu Kusini.
Utiaji saini mikataba miwili kati ya Wakala ya Barabara (TANROADS) na Mkandarasi wa Ujenzi pamoja na Mhandisi Mshauri umefanyika leo Septemba 21, 2024 katika Uwanja wa Samora Mkoani Iringa na kushuhudiwa na Waziri wa Ujenzi Innocent Bashungwa, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu William Lukuvi, Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Pindi Chana, Naibu Waziri wa Uchukuzi, David Kihenzile pamoja na viongozi wa CCM, Serikali na Wananchi wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa Peter Serukamba.
Akizungumza na wananchi, Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa amemuagiza Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Barabara (TANROADS) kuhakikisha anamsimamia Mkandarasi kampuni ya CHICO aliyeshinda zabuni, kutekeleza ujenzi wa barabara hiyo kwa ubora na viwango na kukamilisha kazi ndani ya muda kwa mujibu wa mkataba.
“Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan anatambua barabara hii ikijengwa itafungua fursa za Kiuchumi na Kitalii kwa wana Iringa na ametoa fedha maalum kiasi cha shilingi Bilioni 142.56 ambayo itawezesha barabara kuanza kujengwa mpaka kukamilika fedha inatiririka tu“, amesema Bashungwa.
Bashungwa ameitaja mikakati ya Serikali kwa Mkoa wa Iringa ikiwa ni kuanza manunuzi kwa ajili ya kujenga barabara ya mchepuo ya Iringa - Iringa Bypass (km 7.3) pamoja na kuendelea na upanuzi wa mlima kitonga ambapo tayari kazi inaendelea katika kona 5 hatarishi na ujenzi umefikia asilimia 65.
Akitoa taarifa, Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara (TANROADS), Mhandisi Mohamed Besta amezitaja Kampuni zilizoshinda zabuni za ujenzi ambazo ni China Henan International Corperation (CHICO) pamoja na Mhandisi Mshauri Conseil Ingenierie Et Recherche Appliquee (CIRA SAS) ya Mali kwa kushirikiana na NIMETA Consult ya Tanzania ambapo utekelezaji wake ni miezi 24.
Wizara ya Ujenzi