Mkalukungone mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 862
- 1,755
Mbunge wa Mlimba, Godwin Kunambi amesema baadhi ya Wakuu wa Mkoa na Wakuu wa Wilaya wamekuwa na vitendo vya kukamata Wananchi bila sababu ya msingi.
Ameeleza jambo hilo limetokea katika jimbo lake la Mlimba ambapo Mkuu wa Wilaya wa Kilombero tarehe 26 Agosti, 2024 Kata ya Mbingu kijiji cha Chiwachiwa akienda kusikiliza mgogoro wa ardhi baina ya msitu wa hifadhi ya TFS na wanachi wana Kijiji wa Chiwachiwa.
Akiwa katika mkutano wa ardhi Diwani alileta hoja ya kwamba DC kuthibidtisha mipaka Wananchi wanaamini bado wapo kwenye eneo lao sahihi. Hoja hii ilimpelekea DC kusema unaniharibia mkutano kamata ndani Mtendaji wa Kata, Mtendaji wa Kijiji, Mwenyekiti wa Kijiji na baadhi ya Wananchi 11 hadi sasa wapo ndani.
Inasemekana walipokuwa katika mkutano wa hadhara alipokea simu ya Mkuu wa Mkoa aliweka loundspeker kwahiyo maelekezo ya Mkuu wa Mkoa na DC wakakubaliana kukamata watu 11 wakiwemo watu wanne akiwemo Diwani. Vitendo hivi vimekuwa vya kawaida kwa Mkuu wa Wilaya.